In Summary

• “Ukiona mume anajieleza sana, kupita kiasi, kwa mkewe huenda kweli 'kapiga' nje, na vice versa,” Salim Kikeke aliandika.

Salim Kikeke aondoka BBC baada ya miaka 20.
Image: Facebook

Aliyekuwa mtangazaji wa runinga ya BBC Swahili kwa muda mrefu, Salim Kikeke ameibuka na ushauri au tuseme angalizo la kuchekesha mitandaoni.

Kikeke ambaye aliondoka BBC hivi karibuni baada ya kuwa mtangazaji wao kwa takribani miongo miwili, safari hii amerudi na ushauri kwa watu walioko kwenye ndoa.

Kulingana na Kikeke, ukiona mpenzi wako anajieleza sana baada ya kumuuliza kitu, basi jua kuna uwezekano mkubwa kwamba huenda amecheza mechi nje ya ndoa.

Ukiona mume anajieleza sana, kupita kiasi, kwa mkewe huenda kweli 'kapiga' nje, na vice versa,” Salim Kikeke aliandika.

Mashabiki wake walivalia njuga suala hilo wakisema kuwa ni kweli hata ukiona serikali inatumia nguvu nyingi kujieleza au kutetea kitu basi jua kuna mapungufu yake ambayo wanataka kuyaficha.

Kwa mfano nchini Kenya, kuna mswada tata wa fedha mwaka 2023 ambao serikali imetumia nguvu na jitihada nyingi kuusukuma, huku kwa upande mwingine idadi na makubwa mengi ya wananchi wamekuwa wakipinga mswada huo.

Mashabiki wa kutoka Kenya walitumia huu kama mfano hai wakisema kwamba jinsi serikali inavyotumia nguvu kusukuma mswada huu kupitishwa licha ya wananchi kuwa kinyume nao, huenda kuna kitu ambacho si kizuri kinajaribu kufichwa.

 

View Comments