In Summary

•  Mchekeshaji huyo aliyegeuka kuwa mchekeshaji alimshukuru Lynne kwa kumfanya kuwa baba, baada ya kuishi duniani kwa miaka 41.

Eric Omondi ampa mpenziwe zawadi ya kusukuma mtoto, wawili hao waitarajia mtoto wao wa kwanza.
Image: Instagram

Siku chache tu baada ya kutangaza kuwa wanatarajia mtoto, Eric Omondi ameshaonesha fadhila zake kwa mpenzi wake wa muda mrefu Lynne kwa kumnunulia zawadi ya ‘kusukuma mtoto’.

Lynne kupitia Instagram yake alipakia picha yake akiwa amesimama kando ya gari jeusi na kusema kuwa ni zawadi alipoyokezwa na mpenzi wake mwanaharakati Eric Omondi, huku anaposubiria miezi tisa kutimia na kwenda leba ‘kusukuma mtoto’.

Lynne alisema kuwa mpenzi wake alimpa zawadi hiyo na alikuwa anajivinjari nayo, akitarajia kumpakata mtoto wake wa kwanza, ikizingatiwa kwamba miezi kadhaa iliyopita wawili hao walivunjika mioyo kwa kuharibikiwa na mimba ya mtoto ambaye angekuwa wao wa kwanza.

“Ninafurahiya kawaida na Zawadi Yangu ya Kusukuma🎁” Lynne aliandika.

Wiki jana, Omondi kupitia ukurasa wake alitangaza kwa ushahidi wa picha kuwa wanatarajia mtoto wao wa kwanza, akijilinganisha na kujifananisha na hadithi ya Abrahamu baba wa Imani kutoka kwenye Biblia na mkewe Sarah ambao walilazimika kusubiri kwa miaka ingi kabla ya kupata mtoto wao wa kimiujiza, Isaka.

“Ninahisi kama Sara wa Abrahamu anayetajwa katika Biblia, alingoja maisha yake yote kupata mtoto wake mwenyewe,” Omondi aliandika.

 Mchekeshaji huyo aliyegeuka kuwa mchekeshaji alimshukuru Lynne kwa kumfanya kuwa baba, baada ya kuishi duniani kwa miaka 41.

“Imenichukua miaka 41 lakini hatimaye Mungu amenibariki na zangu. Tunda la viuno vyangu. Asante mpenzi kwa kunifanya baba❤❤🙏🙏. Na kwa Mungu asante kwa kuturudishia mtoto wetu,” Omondi alisema.

Mwaka jana, wapenzi hao kwa mioyo iliyovunjika vipande vipande walitangaza kuharibikiwa kwa mimba yao, jambo ambalo hata hivyo wengi walionekana kutoamini kwa jinsi walifanya, wakimtuhumu mcheshi huyo kwa kufanya sarakasi na mambo mengi mpaka kuwachanganya watu kutojua wakati tukio ni la kweli.

View Comments