In Summary

• Mama huyo alisema kipindi ananyonyesha mwanawe wa kwanza, aikuwa na maziwa mingi na alimnyonyesha kwa miaka 2.

• Alisema kwa sasa anapata maziwa yasiyozidi kiwango cha mililita 50.

Amber Ray alia kukosa maziwa ya kunyonyesha mtoto wake.
Image: Instagram

Mwanafasheni wa mitandaoni, Amber Ray amerudi kwa mashabiki wake mitandaoni akiuliza njia mbadala ya kuhakikisha kwamba mama anapata maziwa ya kutosha kwa ajili ya kumnyonyesha mtoto, baada ya kugundua kwamba hana maziwa ya kutosha kunyonyesha bintiye mwenye umri wa mwezi mmoja.

Amber kupitia Instastory yake aliuliza kama kuna njia inayoweza kumsaidia kupata maziwa ya kutosha huku akisema kuwa hali ya kukosa maziwa imemtokea tu katika binti yake na Rapudo.

Amber alisema kuwa wakati alikuwa akimnyonyesha mtoto wake wa kwanza, Gavin miaka 13 iliyopita, alikuwa na maziwa ya kutosha na alikuwa anatarajia hivyo kwa bintiye Africana, lakini amepigwa na butwaa kugundua hana maziwa ya kutosha.

“Kunayo siri yoyote ya mama kupata maziwa ya kutosha kwa mwanawe? Nilifurahia kumnyonyesha mtoto wangu wa kiume kwa miaka 2 na nilikuwa nategemea kufanya hivyo kwa binti yangu lakini sema kukatishwa tamaa…” Amber Ray alisema.

 Mwanasosholaiti huyo ambaye amekuwa akionekana mitandaoni licha ya kuwa mama mwenye mtoto mchanga alitania kuwa pengine ni kutokana na mtoto huyo mdogo kuwa wa tajiri, akiibua dhana kuwa pengine watoto wa matajiri huwa hawapendi maziwa ya mama.

“Ama watoto wa matajiri hawapendi kunywa maziwa ya mama,” Amber Ray aliuliza.

Mrembo huyo alisema kuwa mpaka kufikia kuulizwa swali hilo, ni hali ambayo imemtia wasiwasi sana kiasi kwamba ametumia vyakula, tembe za maziwa lakini hajafanikiwa kupata maziwa ya kutosha kwa mwanawe.

“Nimejaribu kila kitu kutoka kwa chakula, tembe lakini maziwa mingi kabisa yanakuja ni 50ml. na nyinyi kina mama mnaonyonyesha ni nini mnatumia? Siri ni gani? Kwa sababu kitu tofauti ya ajabu ni kwamba kifungua mimba wangu nilikuwa na maziwa mingi sana,” Amber alisema.

Ray alijitania kwamab pengine amefika umri wa kina mama kutoweza kupata mtoto.

 

View Comments