In Summary
  • Katika chapisho refu, Esma Platnumz alikuwa amejawa na furaha  kwani aliadhimisha miezi miwili ya kuwa kwenye uhusiano naye.
Mjasiriamali Esma Khan, dada mkubwa msanii Diamond Platnumz
Image: Instagram

Esma Platnumz, dada mkubwa wa mwanamuziki maarufu nchini Tanzania Diamond Platnumz kwa sasa anatoka kimapenzi na kijana mdogo  (ben 10).

Mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 37 alifichua hili katika chapisho la hivi punde kwenye akaunti yake ya Instagram, ambapo aliweka wazi kuwa anajivunia uhusiano wao.

Katika chapisho refu, Esma Platnumz alikuwa amejawa na furaha  kwani aliadhimisha miezi miwili ya kuwa kwenye uhusiano naye.

Mama huyo wa watoto wawili mwenye mapenzi tele pia alifichua kuwa alikuwa tayari kupata mtoto naye, na zaidi akawataka wenye chuki wasitamani uhusiano wao ufeli.

Esma alionekana kuwafokea wakosoaji wake kwa madai kwamba uhusiano wake na mpenzwe hautadumu.

"Mrs Rasheed anasherekea kutimiza miezi miwili na mpenzi wake Sitaki nishauriwe hata na ndugu Mmakonde wangu ndo nishampenda na nazaa nae Inshallah…

Kibenten changu, hana hela wangu sijamuomba mtu pesa mnikome wenyewe tunajua tunavyoishi Nampenda na natamba nae sina wa kushare nae sijamkuta na mke nimemkuta yupo Singaliii na stress zake za kuachwa na mimi na zangu tukachanganya tukapata True Love la kimakonde na la kimanyema raha tuu 👌🤣Kifupi msituombee kuachana maana tumelishana Yamini 😋,"Esma alisema.

Hivi majuzi, dada huyo wa Diamond alidaiwa kuwa kwenye mahusiano na Harmonize kutokana na uhusiano mzuri ulioonekana baina yao.

Mwezi uliopita Konde Boy alibainisha kuwa dada huyo wa hasidi wake mkuu aliweka sauti yake kwenye korasi ya wimbo wake  na DJ Seven 'Say Yes' na kumsifia sana huku aitaja sauti yake kama ya kupendeza.

"Eid Mubarak watu wangu wimbo wa  @djsevenworldwide ft Single Boy  & Esma  #SAYYESS umetoka. Sasa sikutaka kusema hili lakini lazima nimtambue malkia. Hizo sauti za kike za chini zilizo pendezesha hapo kwenye baby kitendawili,, Tega!! Naziona Popo Mbili.. Macho Esma alifanya," aliandika kwenye Instagram.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide alimshukuru Esma kwa kuchangia kwenye wimbo huo na kwa upendo na urafiki wao.

 

 

View Comments