In Summary

• Jenifer Jovin ni Mtanzania anayeishi Dar es Salaam, Tanzania, ambaye anafanya vizuri katika biashara, mitindo, na kusomea uanahabari.

• Mapato kutokana na mauzo ya Jezi haya yalisemekana kuwa yataenda kwenye bili za matibabu kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.

Mtu pekee ambaye Alikiba amemfollow
Image: Instagram

Mwimbaji wa Bongo Fleva Ali Kiba amezua gumzo baada ya kumfollow mtu mmoja ghafla kwenye akaunti yake ya Instagram.

Mwimbaji huyo wa Mahaba ana wafuasi milioni 9 lakini hakuwahi kumfollow mtu yeyote mpaka sasa.

Mtu huyo mwenye bahati ni mwanamke anayeitwa Jeniffer Lovin. Kulingana na wasifu wake, Jenifer Jovin ni Mtanzania anayeishi Dar es Salaam, Tanzania, ambaye anafanya vizuri katika biashara, mitindo, na kusomea uanahabari.

Pia Jenifer amemfollow na kushiriki picha na video kadhaa za hao wawili wakifanya video nzuri za kutangaza jezi za soka.

Kiba ni mpenda soka naye Niffer ni mfanyabiashara anayeuza jezi za soka za matangazo kabla ya mashindano yatakayofanyika baadaye wiki ijayo.

Wanamitandao walionekana kupendezwa na video zao nzuri na kujibu wakisema kuwa wawili hao wanapendeza pamoja.

Niffer pia anaonywa kuhusu tabia mbaya za Ali Kiba za kuwa na wanawake.

Katika moja ya video hizo, kemia yao inaonekana kuwa iko wazi kwa wakwe zao mtandaoni.

Anampiga Alikiba kimchezo anapoiga sauti yake.

“NI NAMNA HUYU ANAVYOJARIBU KUNAKILI NAMNA NINAVYOZUNGUMZIA😂😂😂 nipewe maua yangu hii kazi si rahisi.

Hata hivyo karibuni dukani jaman,kama ulikosa jezi tumeongeza tena ,karibuni sana sana," aliandika Niffer kwa mbwembwe

Mapato kutokana na mauzo ya Jezi haya yalisemekana kuwa yataenda kwenye bili za matibabu kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.

"Kama tuvafoham @officialalikiba pamoja @samagoal77 wana misingi yao inayojulikana kama @samakibafoundation Ambayo sasa imeandaa mechi siku ya tar 20/06/2023 na lengo la match hii ni kupata fedha ambayo itaenda kusaidia watoto njiti (wanaozaliwa kabla ya muda wao wa kuzaliwa) ili kuweza kuishi" Jeniffer aliwafahamisha wanamtandao.

Wanamitandao walitoa maoni tofauti tofauti kuhusu wawili hao.

"Hiii mbonaa imeenda🔥🔥, hapa sasa ndo kama mtuletee reality show hivii😂😂😂. Tabasamu na kila kitu ni safi kweli, nimetizama zaidi ya mara kumi sasa❤️," mchome____lingeries aliandika.

"Na kiuno kashika kweli kiba ni malaya mkuu 😂," kariakoo_nightwear aliandika.

"HII IMEENDA TAYARI 👏👏👏," millardayo_ aliandika.

"Mapenzi ni kitu kizuri😍 mambo ya tangazo mi siyajui maoni yangu isiguswe🏃🏼‍♀️," massawe.sharon aliandika.

View Comments