In Summary
  • Wengi walikuwa wakitoa maoni yao wakimuongelea Eddy Nderitu na alichomfanya Eddy ajisikie kwa kumchukua mumewe.
Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Karen Nyamu ni mwansiasa anayejulikana sana mitandaoni, kutokna na drama iliyozunguka uhusiano wake na msanii wa mugithi Samidoh.

Drama hizo zilianza kwani licha ya Samidoh kumuoa  Eddy Nderitu amezaa watoto wawili na Karen Nyamu.

Karen alichapisha kwenye Facebook akisema kuwa chochote kinachoanza na hasira huishia kwa aibu.

Wengi walikuwa wakitoa maoni yao wakimuongelea Eddy Nderitu na alichomfanya Eddy ajisikie kwa kumchukua mumewe.

Hii ilionekana kumkasirisha Karen ambaye aliongeza maoni kwenye chapisho hilo dakika chache zilizopita akiwahutubia wafuasi wakimtaka aachane na Samidoh.

Karen Nyamu aliwaambia wafuasi kwa nini wanajali misimu katika maisha yake kama vile hawana misimu yao pia.

Aliendelea na kuuliza kama ataacha kumpenda Samidoh wanafikiri atakuwa na chochote cha kupoteza katika misimu yake yoyote ya maisha.

"Mbona hujali misimu yangu kama huna misimu yako pia hehehehe nikiwacha kumpenda unaona nitapoteza nitapoteza chochote katika msimu huo,"Karen aliuliza mmoja wa mashabiki wake.

Siku ya Jumapili, seneta Karen Nyamu alichapisha picha yake akiwa amevalia sweta lenye jina la mzazi mwenzake, Samuel Muchoki almaarufu Samidoh.

Wengi wa waliotoa maoni walionekana kuangazia zaidi ujumbe kwenye sweta ya seneta huyo wa kuteuliwa kuliko kitu kingine chochote.

Baadhi ya wanamitandao walidai kuwa alitoa chapisho hilo kama njia ya kumchokoza mke wa Samidoh huku wengine hata wakichukua hatua ya kumuuliza kwa nini aliweka picha hiyo na ikiwa alifanya hivyo kwa makusudi.

"Lakini unaweza ukajiuliza kwa nini jamaa ambaye jina lake linaonekana kwenye sweta yako hakukuoa badala ya mwanamke anayedaiwa kuolewa rasmi naye. Hukuzaliwa jana. Wewe ni mpango wa kando punguza kasheshe," shabiki mmoja alimwambia.

Karen Nyamu ambaye kuwa na ujasiri mwingi ifikapo ni kujitetea alijibu , "Hahaha hatulalamiki punguza umama."

 

 

 

View Comments