In Summary
  • Kamene Goro alicharuka vikali mithili ya mbogo baada ya mwanabogu kutaka kujua kuhusu idadi ya wanaume ambao ametoka nao kimapenzi mapema wiki hii.
Kamene Goro na mchumba wake Deejay Bonez walifunga ndoa siku ya Alhamisi, Aprili 21.
Image: HISANI

Kamene Goro mnamo Ijumaa alifichua kuwa wanaume kadhaa walivutiwa na mumewe DJ Bonez walipokuwa wakichumbiana.

Akiongea kwenye podikasti yake na Oga Obinna, Kamene alikumbuka jinsi mwanamume mmoja alivyowakaribia wakati wa likizo na kuanza kumpongeza mume wake.

Kauli hiyo ilimkera sana Kamene na kujiuliza mtu huyo anataka nini kutoka kwa Bonez.

"Kweli nilipoanza kuchumbiana na Bonez, wanaume wengi walikuwa wanammezea mate Wanaume wengi walikuwa wakimpenda Bonez. Mpaka kuna mwingine akakuja kuniambia tukiwa Mombasa akisema, 'eeh lakini huyu DJ Bonez ni mcute'.

“Akaniambia mara moja, mara mbili mara ya tatu nikamwambia oya skiza, nikauliza unataka nini sasa, unataka tupigane? Mbona unaniambia yeye ni mrembo. Mimi niko hapo, dem wa Nairobi, unafikiri sijui ni mrembo," alisema.

Ufichuzi wa Kamene ulijiri  tu baada ya Kamene kumuuliza Oga Obinna kuhusu jinsia yake.

Kamene na DJ Bonez walifunga ndoa Aprili 20, 2023, katika hafla ya mwaliko pekee. Wenzi hao walikuwa wameishi pamoja kwa miaka miwili lakini walikuwa wamefahamiana kwa zaidi ya miaka sita.

Kamene Goro alicharuka vikali mithili ya mbogo baada ya mwanabogu kutaka kujua kuhusu idadi ya wanaume ambao ametoka nao kimapenzi mapema wiki hii.

Goro kwa uso uliotandwa hasira kote, alimtaka mwanablogu huyo kumpa heshima yake kama mke wa mtu.

“Siwezi nikazungumzia vitu kama hivyo sasa, naomba mnipatie heshima kama mke wa mtu. Na pia ni vibaya sana kuniuliza swali kama hilo wakati mume wangu ameketi hapa kando yangu. Nakuomba unipe heshima sawa na ile ambayo nimekupa leo. [Huyu] amenibooh,” Kamene alisema kwa kughadhabishwa.

View Comments