In Summary

• Mwanamuziki huyo alifichua kuwa alikuwa akitumia usafiri wa umma kwa wakati huo na ata alikuwa ametembea kutoka jiji kuu hadi pahali usaili huo ulikuwa ukifanyika.

• Jua Calli amekua akielezea safari yake katika muziki wa aina ya Genge ambapo Wakenya wengi humchukulia kama mwanzilishi wa muziki huo nchini Kenya.

Image: INSTAGRAM/JUA CALLI

Mwanamuziki wa Genge Paul Julius anayefahamika kwa jina ya usanii kama Jua Cali amehadithia kisa kimoja alipokuwa akiaanza taaluma yake ya muziki wa Genge.

Jua Cali alidhihakiwa alipoalikuwa kuhudhuria mahojiano ya kuweza kujuimuishwa katika kampeni ya kufanya mauzo ya kampuni moja hapa nchini.

Katika mohojiano hayo, swala tata ilikuwa msanii huyo kukosa kumiliki gari.

“swali la kwanza niliulizwa ‘what car do you drive?’ sikutarajia swali hilo lakini nilijibu swali hilo kwa ukweli kwani sikuwa namiliki gari wakati huo.”

Swali hilo lilimshinda kujibu na alishangaa ni kwa nini aliulizwa swali hilo na kulikuwa na uhusiano gani kati ya kampeni hiyo na yeye kumiliki gari.

Mwanamziki huyo mwenye umri wa miaka 43 alifichua kuwa alikua akitumia usafiri wa umma kwa wakati huo na ata alikuwa ametembea kutoka jiji kuu hadi pahali mahojiano hayo yalikuwa yakifanyika.

 Jua Cali alivunjika moyo na iliwalazimu mama yake na mama ya msanii mwenzake wa Calif Records Clemo kumtia moyo.

Baada ya miaka miwili ya kubanduliwa inje katika kampeni hiyo, Jua Cali aliweza kupata nafasi kama balozi wa kampuni ya Motorolla.

Jua Cali amekua akielezea safari yake katika muziki wa aina ya Genge ambapo Wakenya wengi humchukulia kama mwanzilishi wa muziki huo nchini Kenya.

Muziki wa Genge umeweza kujumuishwa katika tuzo za kifahari za Grammy katika kitengo kipya kitakachozitambua muziki kutoka bara la Afrika.

Jumatano Chuo cha Kurekodi cha Tuzo za Grammy kilitoa tangazo muhimu ambalo lilileta msisimko katika sekta ya muziki kote Afrika.

Tuzo za Grammy za 2024 zitakuwa na vipengele vitatu vipya, huku kinachotarajiwa zaidi kikiwa "Best African Music Performance." Kitengo hiki kitasherehekea miziki zitakazoonyesha utamaduni na maisha ya Afrika.

Kitengo hiki kipya kinajumuisha aina mbalimbali za muziki, zikiwemo Genge, Afrobeat, Afro-fusion, Afro-Pop, Alte, Amapiano, Bongo Flava, Kizomba, Chimurenga, High Life, Fuji, Kwassa, Ndombolo, Mapouka, Ghanaian Drill, Afro- House, Hip-Hop ya Afrika Kusini, na Ethiopia Jazz.

View Comments