In Summary

• Fatxo alisema kuwa nia yake kwa Jeff haikuwa mbaya kwani lengo lake lilikuwa kumshika mkono ili wakue pamoja kama vijana.

• Msanii huyo pia alipuuzilia mbali kwamba wakati wa zogo hilo lililochukua miezi kadhaa alikuwa amejificha.

Fatxo asema kuwa nia yake kwa Jeff haikuwa mbaya kama ambavyo wengi walidhani.
Image: Facebook

Msanii na mcheza santuri wa Mugithi DJ Fatxo kwa mara nyingine amesisitiza kwamba hakuhusika kaitka kifo cha ghafla na chenye utata cha Jeff Mwathi ambaye wengi walimtambua kama mbunifu wa mapambo ya ndani.

Akizungumza katika mahojiano na mchekeshaji Obinna, Fatxo alisisitiza kwamba watu wengi walijaribu kuboronga ukweli ulioko n kujaribu kumuonesha kuwa ni mhusika katika kifo cha Jeff, huku akisisitiza kwamba nia yake kwa kijana huyo ilikuwa nzuri tu.

Kulingana na Fatxo, watu wengi walikuwa wanamuita Jeff kuwa ni mbunifu wa mapambo ya ndani licha ya kuwa kijana huyo hakuwa amewafanyia watu wengi kazi hiyo ya kumtambulisha kwa watu wenye ushawishi mkubwa kama yeye.

Msanii huyo alisema kama anadanganya, basi angependa kuona mtu yeyote ambaye aliwahi kuwa mteja wa Jeff katika kufanyiwa kazi ya ubunifu wa ndnai kujitokeza.

“Nyinyi wote mlimuita Jeff mbnifu wa mapambo ya ndani. Mimuita hivyo. Naeza taka tuambiwe mtu mmoja atokee aseme, mimi nishaiundiwa duka na huyu. Sasa huyo interior designer,” Fatxo alisema.

Msanii huyo alisema kuwa aliamua kujihusisha au kufanya kazi na kijana huyo aliyekuwa anachipukia katika taaluma hiyo pasi na kujulikana, kwa sababu alipendezwa naye na alikuwa anafanya kumuinua kijana mwenzake tu.

“Only that for me alikuwa ashaniambia kitambo nikinunua viatu kwa shop yake. Aliniambia: Na hii shop ni mimi nimeunda. Ukitaka kuset kaplace kama haka, nitakuundia. So time nilifika nikaona God amenisaidia naweza weka kajob ka viatu, si ndio nafikiria, yeah I remember a guy.. and he is the right guy wa kunifanyia nini…. Juu to be honest kama huna project, kama hujawahi kuwa na project, nikuulize kuhusu interior designer, unaweza jua?” Fatxo alimuuliza Obinna. “Si utaanza kutafuta, kwanza unafikiria mwenye ako kwa mind, na hicho ndicho nilifanya juu ni kijana mdogo, mkue tu, mkue pamoja,” aliongeza.

Msanii huyo pia alipuuzilia mbali kwamba wakati wa zogo hilo lililochukua miezi kadhaa alikuwa amejificha.

Fatxo alisema kuwa nyumba yake ilikuwa imefungwa na kipindi hicho chote alikuwa anaishi na rafiki yake ambaye alisema hangeweza kumtaja jina kwa vile hapendi mambo ya mitandaoni.

 

View Comments