In Summary

• "Naona Wanamuziki/Wachekeshaji Walioimarika Na Wacheshi Wengi Wanawaendesha. 😔 😟 Na Hiyo Sio Ninachotaka Kwa Brand Yangu..." - Pozee aliandika.

Willy Paul atangaza kuyatupa magari yake aina ya Mercedes.
Image: Instagram

Msanii anayejiita tajiri nchini Kenya Willy Paul ametangaza kuyatupa magari yake mawili aina ya Mercedes akisema kuwa ameamua kufuata uamuzi huo baada ya tathmini ya muda mrefu SANA.

 Kwa mujibu wa msanii huyo, hawezi tena kuendelea kuyatumia magari hayo mawili katika kile aliyataja kuwa ni magari yanayotumiwa na wasanii wanaofanya mzaha katika tasnia ya muziki, na yeye akiwa kama msanii ambaye hazengui katika kazi ya muziki, ameona ni vyema kuyatupa ili kujiunga kwenye ligi ya wasanii wenye heshima.

Pozee, kama anavyojiita, alifichua kwamba magari hayo yake mawili aliyapa majina ya wasanii wakubwa wa kimataifa, Rihanna na Beyonce.

“Nimeamua Kutupa Mitambo Yangu Miwili Mikubwa, Rihanna Na Beyonce, kwaheri kwa familia yangu ya Mercedes. Natamani Ningeyaweka Lakini Waaah...” Pozee alisema.

Msanii huyo alisema kuwa maekuwa akizunguka kila kona na anaona watu aliowataja kuwa wenye mzaha na wachekeshaji ndio humiliki magari hayo, na hivyo kumpa kichocheo kikubwa kuyatupa.

“Kila Kona Ninapogeukia Naona Wanamuziki/Wachekeshaji Walioimarika Na Wacheshi Wengi Wanawaendesha. 😔 😟 Na Hiyo Sio Ninachotaka Kwa Brand Yangu... Kumbuka Daima Kuwa Niliwapenda Lakini Watani Waliwapenda Zaidi. Kwaheri!” Pozee aliandika ujumbe kwa magari hayo yake.

Moja ya gari ambalo msanii huyo analitupa ni Mercedes Benz ambalo alinunua mwishoni mwa mwaka jana kama zawadi ya kujishukuru kwa kutokata tamaa licha ya kulimbikiziwa maneno mengi yaliyolenga kumchafulia chapa yake lakini pia picha katika tasnia ya muziki.

Pozee alisema kuwa mwaka 2022 ulimkubali pakubwa, ambapo ngoma zake Zaidi ya tatu zilipata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki na hivyo kumuingizia hela ndefu, hivyo kulikuwa na haja kubwa ya kujizawadi.

View Comments