In Summary

• Embarambamba alisema ilikuwa njia mojawapo ya njia ya wasanii kutafuta hela katika taaluma yao ya muziki na kuweza kuongeza umaarufu.

• Kwa muda sasa wanuame kuvalia nguo za wanawake umeshrikishwa na watu wanaohusika katika mapenzi ya jinsia moja, LGBTQ.

Image: INSTAGRAM// EMBARAMBAMBA

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Christopher Musyoma almaarufu Embarambamba ameelezea sababu ya kuvalia mavazi ya wanawake.

Akizungumza na Spm Buzz, Embarambamba alisema ilikuwa njia mojawapo ya njia ya wasanii kutafuta hela katika taaluma yao ya muziki na kuweza kuongeza umaarufu.

"Hapa ndio tumefika kama wasanii, unajua lazima tutafuta vile tutakula na vile tunatambaza jina."

Jumatatu mwimbaji huyo anayezingirwa na utata mwingi alionekana akidensi na kucheza kwa njia ya kustaajabisha huku akiwa amevalia rinda fupi na blauzi nyekundu.

Mtunzi huyo wa kinao 'Injili Isonge' pia alionekana akiringa na kujigamba kwa mienendo na kutembea kama mwanamke.

Kwa muda sasa wanuame kuvalia nguo za wanawake umeshrikishwa na watu wanaohusika katika mapenzi ya jinsia moja, LGBTQ.

Lakini baba huyo wa watoto watano alikana madai hayo akisema kuwa hii ilikuwa njia ya kuwatumbuiza wafuasi wake na kuita mtindo yake 'comdey gospel'.

"Waapi, sijaingia LGBTQ, hii inaitwa the best gospel artist people love these days, Embarambamba the best comedy gospel.” Embarambamba alikana madai ya kuhusika kwenye mapenzi ya jinsia moja.

Video hizo zilizosambaa na kuibua gumzo mitandaoni ziliibua hisia mseto kutoka kwa wanamitandao Wakenya huku wengi wao wakionekana kushangazwa na vituko vya mwanamuziki huyo wa nyimbo za injili.

Kulingana na wafuasi wake, wengi walionyesha kutorithika na mtindo huu mpya wa mavazi wa mwanamziki huyo huku wakisema kuwa msanii wa nyimbo za injili hawapswi kuvaa nguo za jinsia ingine.

View Comments