In Summary

•Willy Paul ameomba kushauriwa kuamua nani miongoni mwa mastaa wa Bongo aliowaorodhesha anapaswa kuungana naye katika sanaa yake ya muziki.

Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL

Aliyekuwa mwimbaji wa nyimbo za injili Wilson Abubakar maarufu Willy Paul ameomba kushauriwa kuamua nani miongoni mwa mastaa wa Bongo aliowaorodhesha anapaswa kuungana naye katika sanaa yake ya muziki.

Siku ya Jumanne, alichapisha video akiwa katika GYM na kusema kuwa akiwa alikuwa anafikiri juu ya hilo.

“Help Me Decide Please, Was At Gym Today And I kept Thinking... Who Should I Collaborate With Next . 1. Diamond 2.Harmonize 3.Marioo 4.Alikiba 5.Bruce Melody 6. Innos B 7. Darassa” Aliposti.

Ambapo katika tafsiri, inamaanisha kuwa, nisaidie katika uamuzi tafadhali, nimekuwa katika GYM leo na nilikaa nikifikiria...Nani ninapaswa kuungana naye katika awamu ijayo, 1. Diamond, 2. Harmonize na wengine.

Willy Paul, alimshirikisha Alaine na kutoa wimbo uliovuma sana miaka sita iliyopita, kibao kinachojulikana kama “ I Do”. Pia ametengeneza collabo na Nandy, Samantha j, Arvil pamoja na Nadia Mukami.

Kumuorodhesha Diamond katika nambari ya kwanza, ina maana kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kujiunga na shirika la WCB Wasafi japokuwa pia baadhi ya wanamuziki hasa Harmonize alijiondoa katika shirika hilo, ambalo nyimbo zake zimevuma sana katika kanda ya Afrika ya kati na Mashariki.

Kulingana na utafiti uliofanywa hapo awali na taasisi ya Charts Tanzania nchini humo, ulionesha kuwa Simba aliongoza katika idadi ya watazamaji wa nyimbo kwa kiwango cha juu, huku wengine Willy Paul aliowaorodhesha wakisalia chini yake.

Ushauri wenu ni upi kwa staa huyo wa Kenya?

View Comments