In Summary

• "Mtu kama huyo ningempiga makofi, ni ile tu heshima namheshimu,” DJ Bonez alinguruma.

DJ Bonez nusura zichapane na Oga Obinna kisa mkewe Kamene kuguswa visivyo.
Image: Screengrab//YouTube

DJ Bonez ambaye ni mume halali wa mtangazaji Kamene Goro ametoa onyo kali kwa mchekeshaji Oga Obinna kwa kujaribu kumshika visivyo na hata kumdekeza Kamene mbele yake.

 Watatu hao walikuwa katika jiko la wanafamilia hao ambao Obinna alikuwa anawafunza jinsi ya kupika omena, baada ya kusutwa vikali mitandaoni kwa kujaribu kuosha kitoweo hicho cha dagaa kwa kutumia sabuni kabla ya kupika.

Obinna alijaribu kumtoa chunusi Kamene kwenye shavu lake, jambo lililomghadhabisha sana Bonez na hata kumkaripia vikali Obinna papo hapo akimwambia kwamba hiyo haikuwa heshima ya kumgusa mkewe shavuni wakati yeye mwenyewe kama mume yuko, na anaangalia.

Bonez baadaye alionesha kuchukizwa kwake na kitendo hicho, akifichua kwamba kama si heshima kidogo aliyompa Obinna, angemla kofi na hata kumfukuza ndani ya nyumba yao.

“Nafikiri kuna washikaji wengine ambao ni washenzi. Sawa Omena amepika vizuri mimi sijakataa, sasa mambo ya kushika shika mke wangu, sijui unampanguza, hiyo ni heshima gani? Mtu kama huyo ningempiga makofi, ni ile tu heshima namheshimu,” DJ Bonez alinguruma.

Alimalizia kwa kumtaka Obinna siku nyingin kujiheshimu na kutambua kwamba sasa kuna mipaka kati yake na Kamene kwani ni mke wa mtu.

“Siku nyingine jiheshimu, sawa. Ukija kwa nyumba za watu, heshimu watu na wake zao. Si unakuja unataka kupapasa mke wa mtu, sijui nini unataka kuona mke wa mtu kwanza. Heshimu watu. Kuwa na utu mwanangu,” alisema kwa lafudhi ya pwani.

Awali, Kamene alikuwa amesema kwamba anampenda sana Obinna lakini alikuwa amekwama kati ya kuweka mipaka kati yao na heshima kwa mumewe, kwani hakuwa tayari kuwapoteza wote.

View Comments