In Summary

• Hii ni licha ya wasanii hao kupiga pesa ndefu kwa ajili ya Lebo ya Konde Gang.

 

Cheed afichua hakuna msanii Konde Gang ambaye anamiliki gari.
Image: Instagram

Cheed, msanii wa zamani wa konde inayosemekana kumilikiwa na Harmonize ya Konde Music Worldwide amefunguka kuhusu wasanii wote wa lebo hiyo, wakiwemo wale waliotoka kama yeye na wale waliosalia, ambaye ni Ibraah pekee.

Kulingana na msanii huyo wa muda mrefu, hakuna msanii wa Konde Gang anayemiliki gari kama amabvyo inaonekana mitandaoni, na kwamba magari yote ambayo wanapewa si ya kwao rasmi.

Kama unakumbuka vizuri kuna kipindi nyuma msanii H-Baba baada ya kuondoka pale aliibua malalamishi kwamba hakuna msanii hata mmoja ambaye alikuwa Konde Gang na alikuwa anaonekana na gari la kwake.

Alisema kuwa wasanii wote walikuwa wanapewa magari ambayo yamesajiliwa kwa jina la kampuni hiyo, na si kwa majina yao kama ambavyo wengi walikuwa wanaaminisha.

Hii ni licha ya wasanii hao kupiga pesa ndefu kwa ajili ya Lebo ya Konde Gang.

Ukweli ulionekana baada ya wasanii kama Anjella na Country Boy kupokonywa magari yao baada ya kukatisha mikataba yao kweney lebo hiyo.

Cheed amerudi na ukweli kama huo ambapo anaonekana kuunga mkono maneno ya H-Baba.

“Hakuna msanii wa Konde Gang ambaye anamiliki gari. Hicho ndicho kitu ambacho unatakiwa ukijue. Sio msanii, sio mfanyikazi, ukikuta gari pale ni la ofisi. Wewe utalitumia kwenda studio, kwenda mahojiano lakini hiyo ni mali ya kampuni,” msanii huyo alisema.

Msanii huyo alikuwa anazungumza kupitia kituo cha redio cha East Africa, na ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kabisa kuweza kuzungumzia suala la kuondoka Konde Gang, ikiwa ni baada ya miezi kadhaa kukaa kimya.

 

View Comments