In Summary

• Mchungaji huyo alisema kuwa hakuna siku pesa zitasalia katika mfuko wa kijana mwenye wanawake wengi na kumtaka kutubu na kumrudia Mungu.

• Pia alimwambia kwamba anachostahili kufanya ni kutubu dhambi zake na kumpa Yesu maisha yake kama anataka kuona hela zake zikifanya kazi za maana.

Mchungaji ashauri wanaume kuwapa wake zao nafasi ya kupiga kelele.
Image: facebook

Mchungaji Daniel Mgogo amewashauri wanaume jinsi ya kuwa na pesa kwenye mifuko yao na kuacha kulia kuwa wanapata hela lakini hawajui jinsi zinavyoyeyuka.

Katika mahubiri yake kwenye kanisa la Deliverance Utawala jijini Nairobi, Mgogo alisema kuwa wengi wa wanaume ambao wanapata pesa ndefu lakini mwisho wa siku kugundua hawana kitu ni wale ambao wana foleni ndefu ya wanawake wenye kiu cha pesa.

Mchungaji huyo katika mahubiri yake alisimulia kisa cha mvulana mmoja aliyempigia simu akimtaka kumuombea kwa kile alisema kuwa maisha yake hayaendi licha ya kupata hela nzuri mara kwa mara.

Alisema kuwa katika kilio cha kijana yule, alikuwa anahisi kwamba kuna mikosi inayomuandama lakini kwa mchungaji Mgogo, ushauri wake ulikuwa si upande wa mikosi.

“Hela haziwezi kuyeyuka kwenye mifuko. Nikamwambia moja kwa moja wewe nahisi kabisa wewe utakuwa mal**a, utakuwa na wanawake wengi,” mchungaji huyo alimlipua.

Alisema kuwa baada ya kutamka hivyo mvulana yule alikubali ni kweli ana wanawake wengi ambao pesa zake nyingi hutumbukia.

“Kama una wanawake wengi, unategemea hea zikae kwenye mfuko, kwa namna gani? Unaanza kutafuta eti wazazi ndio wanakufilisi na kuusahau umala*a wako kwamba ndio unaokufilisi. Wewe unawafahamu hawa viumbe wanaoitwa binti, hawajawahi kuridhika. Wanakukomba halafu bado wanasema hazitoshi,” alishauri.

Pia alimwambia kwamba anachostahili kufanya ni kutubu dhambi zake na kumpa Yesu maisha yake kama anataka kuona hela zake zikifanya kazi za maana.

Mchungaji huyo alitoa onyo kali kwa watu wasio enda kanisani na ambao wanampigia simu wakitaka Baraka za maombi.

“Yaani wewe hujaenda kanisani miaka sita, unaniambia mimi nikuombee, niombe kwa Mungu yupi? Wewe pambana na hali yako,” alisema akisisitiza kwamba watu kama hao wanawafanya wachungaji kuwa kama waganga wa kijiji hali ya kuwa wanafaa kuwa wawakilishi wa Mungu duniani.

View Comments