In Summary

• Obinna alijitolea kumfunza Kamene jinsi ya kupika Omena baada ya kuzua gumzo mitandaoni alipoonekana akijaribu kuosha Omena kwa sabuni kabla ya kupika.

Kamene&Obinna Kamene Goro akiri mapenzi yake kwa Oga Obinna.
Image: Screengrab//YouTube

Mtangazaji Kamene Goro amekiri mapenzi yake kwa mchekeshaji na aliyekuwa mtangazaji mwenza Oga Obinna, licha ya kwamba amefunga harusi hivi majuzi na mpenzi wake wa muda DJ Bonez.

Katika kipindi ambacho Obinna alikuwa alikuwa anamfunza Kamene jinsi ya kupika chakula aina ya Omena, Kamene alisema kuwa anampenda sana Obinna lakini pia kumpa tahadhari kwamba anafaa kuweka mipaka na kufahamu kwamba kwa sasa yeye ni mke wa mtu.

“Leo nina wasiwasi kidogo kuhusu Obinna, nimemjua kwa muda ni rafiki yangu sana, tulifanya kazi pamoja. Lakini ninahisi kwamba anajaribu kung’ang’ana kukubali ukweli kwamba unajua nina mume sasa , nimeolewa….” Kamene alisema.

Alikiri kwamba Obinna alikuwa akijua kwamba yeye na Bonez walikuwa wanachumbiana na pia kujua fika kuwa asingetaka kuchumbiana na mtu mwingine, lakini akasema kuwa licha ya kumpenda Obinna, anafaa aanze kumwangalia kwa jicho tofauti na jinsi alivyokuwa anamuona kipindi wakifanya kazi pamoja.

“Kuna kuzoeana kiasi ambako nahisi anafaa kusonga nyuma kidogo. Ni rafiki yangu, anaweza kuja kwa nyumba muda wowote lakini pia ajue kwamba kuna mwanamume unajua. Obinna kusema kweli nakupenda sana, wewe ni rafiki yangu lakini mimi sasa nimeolewa na kuna vitu ambavyo hufai kufanya kwangu,” Kamene alisema.

Mtagazaji huyo alisema kuwa amesalia kwenye njia panda jinsi atakavyofanya kuhusu baadhi ya matukio ambayo yalichipukia wakati wakiwa jikoni pamoja na Obinna na mume wake, kwani hataki kumpoteza Obinna kama rafiki wake na pia Bonez kama mume wake.

Obinna alijitolea kumfunza Kamene jinsi ya kupika Omena baada ya kuzua gumzo mitandaoni alipoonekana akijaribu kuosha Omena kwa sabuni kabla ya kupika.

 

View Comments