In Summary

• "Kitu kimoja ambacho watu wanafaa kujua ni kwamba ukifanya kitu kwa rushwa ya ngono, hakitokaa kiendelee" - Niffer alisema akipuuzilia mbali madai ya kutoka kimapenzi na Kiba.

Mtu pekee ambaye Alikiba amemfollow
Image: Instagram

Mjasiriamali wa duka la nguo Niffer amefunguka kuhusu sakata la kuhusishwa kuwa kichocheo kikubwa cha mke wa Ali Kiba, Amina Khelef kuibua suala la kutaka talaka kutoka kwa msanii huyo.

Katika mahojiano na blogu moja ya nchini mwao iliyomtembelea katika duka lake la nguo, Niffer alisema alichokifanya ni kumvalisha tu Alikiba tena kwa heshima akiwa anajua fika kuwa ni mke wa mtu.

Mrembo huyo alisema kuwa wasichokijua watu wengi ni kwamba yeye ni mtu ambaye anajiheshimu sana na katu hawezi kutoa rushwa ya ngono ili kupata kitu kutoka kwa mtu ambaye anatakiwa kumvusha kutoka upande mmoja au mwingine, huku pia akisema kuwa wale ambao wamekuwa wakipayuka kuwa Alikiba alimwacha mkewe ili kumpenda yeye hawajui ni jinsi gani msanii huyo anavyompenda mkewe.

“Alikiba nimempa heshimu tu na bidii. Mtu yeyote unayefanya kazi naye, ni lazima uwaoneshe heshima, uheshima faragha yao. Kitu kimoja ambacho watu wanafaa kujua ni kwamba ukifanya kitu kwa rushwa ya ngono, hakitokaa kiendelee. Yaani ukishaanza kujihusisha kimapenzi na watu unaofanya nao kazi, watu wanaotakiwa wakuvushe kutoka sehemu moja kwenda nyingine, hakitokaa kiendelee. Mapenzi yana wivu,” Niffer alisema.

“Mimi ni mrembo nina kila kitu, ukifanya kitu na mtu lazima kuna wale watasema; yaani pale apite hivi hivi, haiwezekani, yaani kuna watu wamekaa kabisa mwamba hawezi vitu vyake vile sijui nini…si hivyo kanisa. Yaani natamani wangekuwa wanajua ni jinsi gani Ali anavyompenda mke wake. Anampenda mkewe sana. Hata kama mkiwa mnafanya kazi, ikifika time ya mke wake amempigia simu, kila kitu kinasitishwa hadi pale ataridhika kuzungumza naye, na ikitokea wamekwazana kidogo, hamtoendelea hadi siku ifuatayo,” Niffer aliongeza.

Mrembo huyo aligonga vichwa vya habari baada ya kuonekana amepiga picha na Alikiba kutangaza jezi zake, na Alikiba alifanya kumtag ikiwa ni nadra sana kwa msanii huyo kumtag mtu mwingine Instagram.

Hilo lilizua gumzo baadhi wakisema kuwa Alikiba amepata mpenzi mpya na siku chache baadae mke wake alicharuka mitandaoni akimzomea msanii huyo kwamba amemfanya mfungwa wake kwa muda mrefu kwa kukataa kusaini karatasi za talaka.

Akiwa nchini Kenya, Alikiba hata hivyo alionesha nia yake kuwa tayari kusaini karatasi hizo, kitu ambacho alikitaja kuwa si shida kubwa.

View Comments