In Summary

• Bendi hiyo ilitaganza mafanukio ya hivi punde ya kundi hilo katika akuanti yake ya Instagram wakielezea furaha yao na shukrani kwa kutambuliwa na akademia hiyo ya kifahari.

• Tangazo hilo linakuja wiki chache tu baada ya chuo hicho cha kurrekodi kuijumuisha muziki wa Genge katika tuzo za Grammy.

Wanamuziki wa bendi ya Sauti Sol.

Bendi ya Sauti Sol kutoka Kenya imetangaza kupewa idhini ya kupiga kura na taasisi ya Kurekodi muziki  ya Grammy.

Bendi hiyo ilitaganza mafanukio ya hivi punde ya kundi hilo katika akaunti yake ya Instagram wakielezea furaha yao na shukrani kwa kutambuliwa na taasisi hiyo ya kifahari.

Kujumuishwa kwa Sauti Sol katika akademia hiyo kunaangazia ushawishi unaokuwa na utambuzi wa muziki wa Kenya kwenye jukwaa la kimataifa.

Katika tangazo lao, bendi hiyo ilieleza furaha yao na kutoa pongezi kwa waimbaji na washirika wa kibinafsi katika kundi hilo kwa kupata mwaliko huo.

"Karibu kwenye Darasa la Chuo cha Kurekodi cha 2023. Hongera @bienaimesol @iamchimano @itsmefancyfingers na @savarafrica kwa mwaliko wao wa kujiunga na @recordingacademy kama Washiriki wa Kupiga Kura," ilisoma ujumbe huo.

Hili ni shirika la wanamuziki, watayarishaji, wahandisi wa kurekodi na wataalamu wengine wa kurekodi waliojitolea kuboresha hali ya maisha na utamaduni kupitia muziki.

Wanachama wa Kupiga Kura wana jukumu kuu la kuweza kuamua wateule wa kila mwaka wa GRAMMY na washindi wa mwisho kila mwaka. Kujumuishwa kwa Sauti Sol kunaleta msisimuko nchini Kenya kwani sasa Wakenya wengi wanatarajia kujumuishwa kwa wasanii wa humu nchini katika tuzo hizo.

Tangazo hilo linajiri wiki chache tu baada ya akademia hiyo kujumuisha muziki wa Genge katika tuzo za Grammy.

Vilevile, wanachama wa  akademia hiyo wanaweza kupendekeza marekebisho kwenye Kanuni na Miongozo rasmi ya Tuzo za GRAMMY, ikijumuisha mapendekezo ya aina mpya za GRAMMY na mabadiliko makubwa kwa vipengele vilivyokuwepo awali.

Kupitia tovuti ya chuo hicho Makamu wa Rais wa  Grammy Kelley Purcell aliwapongeza na kuwakaribisha wanachama wapya pamoja na kundi la Sauti Sol.

"Tunawahimiza wanachama wetu wapya walioalikwa kujiunga na Academy na kushiriki katika kuwahudumia, kusherehekea na kutetea wasanii wenzao mwaka mzima na kuleta mabadiliko katika muziki." Alisema Kelley Purcell.

View Comments