In Summary

• Embarambamba alimsihi mchungaji huyo amhurumie kwa sababu ametumia pesa nyingi kufanya video za nyimbo zake zilizokuwa kwenye akaunti hiyo.

Image: INSTAGRAM// EMBARAMBAMBA

Mwanamuziki wa nyimbo za injili kutoka Kisii,  Christopher Musyoma almaarufu Embarambamba anamsihi Mchungaji Ezekiel kumrudishia akaunti yake ya Youtube.

Mwimbaji huyo akizungumza katika video aliyoweka kwenye akaunti yake ya Instagram alimuomba mchungaji huyo amhurumie kwa sababu ametumia pesa nyingi kufanya video za nyimbo zake zilizokuwa kwenye akaunti hiyo.

"Mhubiri Ezeekiel, nirudishie akaunti yangu tafadhali, nimetumia pesa nyingi kurekodi video kwenye chaneli hiyo na nimepitia shida mingi vile nimelezea. Tafadhali Ezekiel nione huruma vile unataka kuonewa huruma."

Baba huyo wa watoto watano alielezea sababu ya kufungiwa akaunti yake kuwa kuweka video ya mahubiri ya mchungaji tata Ezekiel wa kanisa la New Life Prayer Centre and Church.

"Mhubiri Ezekiel wa Mombasa, kuna mahubiri yako yaliyonifurahisha kutoka kwa chaneli yako nikaona niiweke kwa akaunti yangu, ukaniblock na ukaenda na Youtube yangu"

Embarambamba katika mahojiano na Nairobi News hivi majuzi alifichua kuwa akaunti yake ya Youtube ilikuwa imefungwa na  kulazimika kufungua akaunti mpya ili aweze kuendelea na taaluma yake ya muziki. 

Alizungumzia hii baada ya video aliyopakia kwenye mitandao ya kijamii akiwa anakata kiuno huku amevalia mavazi za kike.

Mwimbaji huyo  mwenye utata alionekana akidensi na kucheza miondoko ya kustaajabisha huku akiwa amevalia sketi fupi la kahawia na blauzi nyekundu.

Video hizo ziliibua hisia mseto kutoka kwa wanamitandao wengi wakihisi mwanamziki huyo mwenye umri wa miaka 35 alienda kinyume na matarajio ya wengi kwa wasanii wa nyimbo za injili.

Embarambamba aidha alijitokeza na kujitetea kuwa alifanya video hizo kama njia moja ya kuweza kujitafutia hela na kuongeza umaarufu wake.

"Hapa ndio tumefika kama wasanii, unajua lazima tutafute vile tutakula na vile tunatambaza jina."

View Comments