In Summary

• Rais huyo wa buradani katika bara la Afrika alisema kuwa anamchukulia Simple Boy kama ndugu yake na kuwa safari yao katika tasnia ya burudani nchini ni miaka nyingi.

Mwanamuziki Stivo simple boy na Erick Omondi.
Image: INSTAGRAM

Mchekeshaji maarufu Erick Omondi amejitokeza na kumsaidi msanii Stevo Simple Boy baada ya mwimbaji huyo kujitokeza na kuomba msaada wa kifedha.

Katika video zilizochapishwa katika chaneli ya mwanablogu Vincent Mboya, mchekeshaji huyo aliwaletea msaada wa vyakula na kusikitikia hali ya mwimbaji huyo maarufu.

“Kuna vitu mob hapa ikiwemo chakula kwa ndugu yangu wa miaka mingi. Nimemletea mafuta, sukari, kuna usalama hapa kwa kuwa kitu ninaenda kumpea inahitaji usalama wa hli ya juu na ni Unga wa kupika ugali”

Rais huyo wa buradani katika bara la Afrika alisema kuwa anamchukulia Simple Boy kama ndugu yake na kuwa safari yao katika tasnia ya burudani nchini ni miaka nyingi.

“Niliona mahojiano yenu,nikaona maneno yake na simple boy ni boy wangu na sai ninapigania haki za wanamuziki na waunda maudhui. Huyu ni ndugu yangu na tumetoka mbali na yeye. “

Katika mahojiano hayo hayo Erick Omondi aliendelea kusihi serikali kuondoa ushuru ya asilimia 5 kwa waunda maudhui ya kidijitali ambayo pia itawaadhiri wanamuziki pakubwa. Erick alisema wasanii tayari wanapitia maisha magumu na ushuru hiyo itaongeza mateso yao pakubwa.

Mchekeshaji huyo ambaye amegeuka kuwa mtetezi wa haki za wanyonge alisema kuwa licha ya chakula aliyompaa ana mpango wa kumzawadi Stivo Simple Boy lakini alikataa kufichua ni nini hicho.

Siku ya Jumamosi, msanii kutoka Kibera alikiri madai ya mkewe kuwa ya kweli kwamba wanateseka sana na muda mwingi huwa wanalala bila kutia kitu chochote kinywani licha ya msanii huyo kuwa na jina kubwa katika muziki wa Kenya.

 “Ni kweli, unajua kwa sababu unajua sina biashara tofauti na usanii, usanii ndio kazi yangu na kama hakuna shoo inabaki tunalala njaa. Hapo naunga mke wangu mkono,” Stevo alisema.

View Comments