In Summary

• Hata hivyo, Anjella alisema kuwa Harmonize alikuwa bosi mzuri ambaye alikuwa anajitoa kwake kwa njia kubwa.

Harmonize adhibitisha kuachana na Anjella
Image: YouTube screengrab

Msanii aliyekuwa chini ya lebo ya muziki ya Konde Music Worldwide, Anjella amefunguka jinsi ambavyo alikutana na Harmonize na hatimaye kusajiliwa na kutambulishwa kwa watu wengi.

Katika mazungumzo na Millard Ayo, Anjella alisema kuwa yeye alianza kama mumbaji wa masokoni tu na wala hakuwa anajuana na Harmonize.

Nyota yake iliangaza tu baada ya Harmonize kuchapisha mitandaoni kwamba alikuwa anatafuta mtu wa kufanya collabo na yeye, na watu wengi walimtag Anjella kwenye chapisho hilo na hivyo ndivyo pia Harmonize alipata kumfuatilia na kumchukua.

“Ilikuwepo kwamba kuna wimbo alihitaji collano, kwa hiyo alisema kwamba watu watag mtu ambaye wanahitaji afanye naye collabo. Kuna mtu alinitag, kwa hiyo yeye akanifuatilia, akanichagua. Niliona mwenyewe Harmonize akiniposti nikawa siamini,” Anjella alisema.

Anjella alisema kuwa hatimaye walikutana na Harmonize na akapewa chumba katika makao ya Konde Village lakini baada ya miezi kama miwili hivi alipata sehemu nyingine akapanga na kuanza kulipa kodi mwenyewe.

Hata hivyo, msanii huyo alisisitiza kwamba hakuwahi kuwa na mazoea na Harmonize wala hawakuwahi kuwa na ushikaji licha ya kwamba alijitoa sana kwake kuhakikisha kwamba anajinafasi kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Flava.

“Bosi alijitoa sana kwangu. Ni mtu ambaye alikuwa anaumiza kichwa kwa ajili ya Anjella. Yaani hicho nilikuwa nasema kabisa kweli bosi wangu ananikubali. Hatukuwahi kuwa na ushikaji wala mazoea na Harmonize hata kidogo,” Anjella alisema.

Msanii huyo alisema kuwa mawasiliano yote yalikuwa yanamfikia kupitia meneja wake na ikitokea ni yeye anamfuata kabisa Harmonize moja kwa moja basi msanii huyo angejua kuna jambo zito.

Mpaka kufikia hatua ya kushindwa kuelewana hadi kuvunja mkataba, Anjella alikuwepo anamuomba meneja wake kuhakikisha amemtengea nafasi ya kukutana na Harmonize moja kwa moja lakini ilishindikaka.

 

View Comments