In Summary

• Awali tuliripoti kwamba msanii huyo alijitokeza na kumpa msanii mwenzake Stevo Simple Boy ushauri wa jinsi ya kufanikiwa katika Sanaa ya burudani nchini.

Mulamwah.
Image: Facebook

Mchekeshaji Mulamwah kwa mara nyingine tena amezungumzia suala la yeye kutomiliki gari licha ya kuwa na jina kubwa kwenye Sanaa ya muziki na pia kupata pesa nyingi ambazo zingine anazionesha kwenye mitandao yake ya kijamii.

Katika mahojiano na SPM Buzz, Mulamwah alisema kuwa yeye bado anazidi kukazana na kujitahidi kadri ya uwezo wake kuunda maudhui mitandaoni katika kile alikitaja kuwa anaidai Sanaa ya uchekeshaji siku moja kumpa uwezo wa kumiliki gari na nyumba.

Mchekeshaji huyo ambaye kwa sasa anaendeleza mjengo wa umba lake la kifahari kijijini mwao Magharibi mwa Kenya alisema kuwa wakati mwingine anawaza sana siku akipata gari atafikiria kufuta akaunti zake zote za mitandaoni.

Aliwaambia mashabiki wake kwamba ile siku watasikia amepata gari basi wako radhi hata kuacha kumsupport.

“Mimi nakuwa nimedai Sanaa tuseme inipatie nyumba unaona, labda ninunue kigari. Sitakuwa nadai Sanaa hii kitu kingine chochote. Wacha masomo yanifungulie biashara nifanye vitu vingine. Mimi siku ile nanunua gari, haki muache tu kusupport Mulamwah, muache tu juu nitakuwa nimeshapata kila kitu,” alisema Mulamwah.

“Kusema ukweli huwa nimepanga yaani kuna siku nitafuta akaunti zote za mitandaoni, sitakuwa. Kwa sababu ile presha nimepitia hapo, mambo mimi hupitia ni mengi.” Alisema, akirejelea kitendo cha kuchoma shati lake miaka michache nyuma wakati alichipukia mitandaoni kama mcheshi.

Awali tuliripoti kwamba msanii huyo alijitokeza na kumpa msanii mwenzake Stevo Simple Boy ushauri wa jinsi ya kufanikiwa katika Sanaa ya burudani nchini.

Mulamwah alimpa Stevo takrima ya shilingi elfu 5 na pia mkewe Grace shilingi elfu 3 na kumshauri kukoma kabisa kuhusisha uongozi katika kazi zake za muziki.

Alisema kuwa yeye yuk tayari kuketi chini na kuzungumza na msanii huyo, mradi tu wapate mwafaka wa kumsaidia na kuona ameinuka kama wenzake, ikiwemo kumsaidia jinsi ya kufungua akaunti ya TikTok ambayo alisma Stevo hana licha ya sauti zake kutumiwa na wakuza maudhui wengi kwenye mtandao huo wa video fupi.

 

View Comments