In Summary

• Simple Boy alisema kuwa Harmonize alitaka kufanya Collabo naye ombi ambalo meneja wake alipinga.

• Mwanamuziki huyo aliongeza kuwa hakufahamu sababu ya usimamizi wake kupinga ombi la Harmonize kufanya kazi naye.

Stivo Simple Boy na Harmonize
Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki anyekumbwa na matatizo ya kifedha, Stevo Simple Boy amefichua kuwa usimamizi wake wa kwanza, Made in Kibera (MIK) , ulumzuia kushirikiana na mwanamuziki maarufu wa nyimbo za Bongo, Harmonize.

Akizungumza siku chache tu baada ya Meneja wake, Men In Business kufutilia mbali mkataba wao na mwimbaji huyo, Simple Boy alisema kuwa Harmonize alitaka kufanya Collabo naye ombi ambalo meneja wake alipinga.

"Enzi zile nikiwa bado Made In Africa, so Harmonize akanipigia simu ili tuweze kufanya collabo na management wakasema hawezi akafanya kazi na Harmonize. Na sikufahamu sababu yao kusema hvyo"

Simple Boy aliongeza kuwa sababu sasa yuko huru bila Meneja alimuomba Harmonize kufikiria kuhusu kufanya kazi naye.

"Lakini kwa sasa hivi mimi niko huru, Harmonize anaeza akafanya kazi na mimi."

Simple Boy alikiri kuwa hangeweza kutoa maoni yake kuhusiana na ombi hilo la Harmonize kwa sababu alikuwachini ya usimamizi na kulingana naye mwanamuziki akiwa chini ya lebo haruhusiwi kutoa maoni yake.

"Unajua ukiwa under management hurusiwi kuongea vitu mingi. nikakubali tu lakini nikasema ipo siku nitafanya kazi na Harmonize."

Jumatatu, mwanamuziki huyo akipokea msaada wa kifedha kutoka kwa mchekeshaji Mulamwah na ni wakati huo alibainisha kuwa sasa atajiwakilisha yeye mwenyewe akisaidiwa na mke wake na marafiki wake watatu.

“Sai mimi nimeamua kuwa meneja kivyangu nikiwa na mke wangu na rafiki zangu watatu pamoja na wakenya wote kwa jumla. Kama mtu anataka kunisupport wakuje kwangu mimi binafsi.”

Stevo Simple Boy alidai kuwa meneja wake wa zamani ,ambaye mapema wiki hii alikatisha mkataba wao, hakuwa akimsaidia katika taaluma yake na alitumia nafasi hiyo kumhujumu.

“Meneja hafanyi kazi nzuri, ukiangalia kwanza Instagram hapost msanii wake anapost msanii mwingine na kumpromote.”

Baadhi ya wakenya na wasanii wenzake katika tasnia pana ya Burudani nchini wamejitokeza kwa sauti moja na kumtetea mwanamuziki huyo ambaye wengi walihisi ni dhaifu na meneja alikuwaa akimnyanyasa.

View Comments