In Summary

• Alisema kuwa kutumia au kutotumia baadhi ya vitu sio kigezo cha kuchagua mtu mzuri wa kukaa naye katika ndoa.

Kamene Goro akiri kuvuta sigara.
Image: Instagram

Mtangazaji maarufu Kamene Goro amekiri kwamba yeye ni mraibu wa kuvuta sigara na kusema kwamba mume wake DJ Bonez huwa anateseka sana na tabia hiyo.

Katika podikasti yake na mchekeshaji Obinna usiku wa Ijumaa, watatu hao walikuwa wanazungumzia suala la wanawake kuvuta sigara na tabia zingine ambazo huwaogopesha wanaume kuwakaribia.

Obinna alisema kuwa mwanamke ambaye analewa sana, anayevuta sigara, bangi na vilevi vingine kamwe hawezi kuwa mwanamke wa kuishi naye kama mama watoto wako.

Kwa upande wake Bonez alisema kwamba hata yeye anachukia sana wanawake wa kuvuta sigara huku akidokeza kuwa ninapitia changamoto kali’ kutokana na tabia ya mkewe kuvuta sigara.

Kamene alikiri ni kweli mume wake anapitia wakati mgumu sana kumudu tabia yake ya kuvuta sigara lakini akasema kuwa tangu wajuane na kuoana miezi miwili iliyopita, amejaribu sana kujidhibiti, akisema kuwa kila mtu ako na tabia zake mbaya.

“Kila mtu ako na tabia zake mbaya, kuna watu ambao hawaogi, kuna wale hawatakatishi nywele zao.. unajua hata mimi niko na tabia zangu mbaya. Kitu ni kwamba, acha tuzidhibiti tabia hizo ili kuwa raia wema. Kama wewe ni msee wa kunywa pombe, si eti unakunywa hadi unajisahau. kama wewe ni mtu wa kuvuta sigara na uko karibu na watu ambao hawapendi, usivute karibu nao,” Kamene alisema.

“Bonez atateseka sana na tabia yangu ya kuvuta sigara, siwezi danganya, huwa navuta sigara. Lakini kusema ukweli nimepunguza kwa kiasi kikubwa tangu tujuane. Siku hizi yaani, pengine niko na msongo wa mawazo, umenikasirisha ama tunapiga sherehe. Hata hapa ndani ya nyumba ni ngumu sana,” Kamene aliongeza.

Pia mtangazaji huyo alisema kuwa hakuna shida na bangi kwa baadhi ya watu huku akisema kuwa kutumia au kutotumia baadhi ya vitu sio kigezo cha kuchagua mtu mzuri wa kukaa naye katika ndoa.

View Comments