In Summary

• Katika moja ya sauti hizo ambayo inaaminika kuwa ya Zari, anasikika akitoa maelekezo kwa promota huyo jinsi atakavyompokea Shakib,

Zari awasuta wanaomkejeli kumuita Shakib Fala
Image: Instagram

Mfanyibiashara Zari Hassan amenyoosha mtutu wa kombora lake kwenda kwa wale ambao wamejitokeza kumsuta vikali baada ya sauti yake kuvujishwa akimuita mumewe Shakib Cham kama fala.

Katika Kiswahili cha Bongo, fala ni mtu ambaye ni kama zamwamwa ambaye hajielewi.

Zari amewajibu kwa shombo vile vile akisema kuwa wanaomzungumzia kwa njia hasi hawana lolote na wanahitaji kichokonoo ili kuliondoa jina lake kwenye midomo yao kwani ni kama limenata katikati ya meno yao.

“Wanahitaji kichokonoo kwa sababu jina langu limekwama kwenye meno yao,” Zari aliandika.

Hii inakuja baada ya promota wake katika shoo iliyobuma ya Uingereza huko Birmingham kuvujisha baadhi ya sauuti ambazo walikuwa wanazungumza na mjasiriamali huyo wa Uganda mwenye makao yake Afrika Kusini.

Katika moja ya sauti hizo ambayo inaaminika kuwa ya Zari, anasikika akitoa maelekezo kwa promota huyo jinsi atakavyompokea Shakib, akimtaja kuwa ni fala ambaye hana ujasiri wa kujibeba mbele za watu.

Hata hivyo siku moja baadae, Zari alionekana kuitetea sauti hiyo akisema kuwa hakuwa analenga kumdunisha mume wake kwenye hadhara na kusema alikuwa tu anatoa maelekezo jinsi atakavyopokeewa ili asije akamuaibisha.

Kwa upande wake, Shakib alionekana kukasirishwa na kitendo cha Zari na kutupa dongo kwake akiandika Instagram kwamba ni kiburi ambacho huenda kitamfanya Zari kumpoteza.

Baadhi ya wanamitandao wamekuwa wakimsuta Zari kwa kumdhalilisha mume wake na hata kuanika udhaifu wake kwenye watu wasiomjua wakisema kuwa hakuna ndoa inayoweza kujenga kwenye misingi hiyo ya mke kuanika udhaifu wa mumewe hadharani.

View Comments