In Summary

• Salasya alimuahidi Stevo kumhamisha Jumatatu – kesho kwenda kwenye nyumba nzuri Nairobi.

• “Kule Oyugis nitakupa nyumba pia kama wale waliokuahidi hawaakupa katika siku 15 zijazo, mimi nitakupa." - Salasya.

MP Salasya kumjengea Stevo Simple Boy nyumba.
Image: Screengrab// YOUTUBE

Mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya hatimaye amekutana na msanii mwenye matatizo na misukosuko mingi kwenye safari yake ya muziki, Stevo Simple Boy.

Salasya alikuwa ameomba kukutanishwa na msanii huyo kutoka Kibera baada ya hadithi yake kuenezwa kuanzia wiki jana jinsi amekuwa akipitia maisha magumu hadi kulala njaa licha ya kuwa na jina kubwa kweney Sanaa.

Baada ya kukutana, Stevo alimwelezea Salasya kwamba matatizo yake yamesababishwa na menejimenti ambayo baadae imekuja kujitoa na kuvunja mkataba wake baada ya mkewe Grace Atieno kuweka wazi kwamba huwa wanalala njaa.

Salasya alimuahidi Stevo kumhamisha Jumatatu – kesho kwenda kwenye nyumba nzuri Nairobi na pia kumuahidi kumjengea nyumba ya kisasa nyumbani kwao Oyugis kaunti ya Homabay, lakini kwanza akamtaka kutupilia mbali wazo la kutafuta menejimenti nyingine yoyote.

“Kitu cha kwanza sitaku sasa uwe na meneja. Nataka ufanye kazi kivyako. Mimi wakati napiga kampeni nilikuwa kila kitu, sikuwa nasimamiwa na mtu,” Salasya alimwambia.

Mbunge huyo alimuuliza msanii huyo angependa kumsaidia kivipi na Stevo akasema kuwa angependa kuhamishiwa katika mazingira mazuri, kujengewa nyumba kijijini lakini pia kufunguliwa biashara.

“Nimekusikiliza, jumatatu utakuwa na nyumba mpya, nitakukodishia, nitakutafutia nyumba hapa Nairobi na nitakulipia kodi ya hadi miezi mitatu hadi uwe imara lakini pia nitakutafutia fenicha, godoro, kitanda na vitu vingine. Halafu pia nataka sasa urudi kwa burudani, utafute matamasha yako mwenyewe, shoo zako na uratibu pesa zako mwenyewe na mapato na uwache kusimamiwa.”

“Kule Oyugis nitakupa nyumba pia kama wale waliokuahidi hawaakupa katika siku 15 zijazo, mimi nitakupa. Kwa sasa tafuta nyumba yenye itakufurahisha, mimi nitafanya upande wangu. Wiki kesho nitakuja hapa nisem nimefanya hiki na hiki na kile ili watu mjue,” Salasya alisema.

View Comments