In Summary

• Kamene alifichua kwamba mpaka sasa ni mwaka wao wa tatu tangu waanze kuchumbiana na mcheza santuri Bonez.

Kamene Goro azungumzia kuolewa na Bonez,
Image: Screengrab

Kamene Goro kwa mara ya kwanza ameonekana kudokeza ni kwa nini alimchagua mcheza santuri Deejay Bonez kama mume wake, licha ya wengi kuhisi kwamba wawili hao hawaendani.

Katika podikasti yao na Obinna, Kamene alisema kuwa alichagua kuolewa na DJ Bonez kwa sababu kwa muda mrefu wanaume walikuwa wanasema kuwa wanawake hawafai kuweza vigezo vya mwanamume ambaye anamtaka katika maisha yake.

Mtangazaji huyo alisema kuwa wanaume ndio wanaweka vigezo vingi kuhusu yule mwanamke ambaye wanamchukulia kama ‘wife material’ ilhali wamekuwa wakiwaambia wanawake kutokuwa na vigezo sawia.

“Wakati mwingine pia nyinyi wanaume mnaitaji kuwa na busara, achana na hii ya ati wife material inakaa hivi, ooh sijui hafai kuvaa jeans yenye ni rugged, ooh havai kuvaa sketi fupi. Wanaume walitumabia kama wanawake tuache kuwa na vigezo. Tunawachukua jinsi mlivyo ndio maana kuna warembo wamependana na wendawazimu, wengine wanachumbiana na wanaume ambao tayari wako kwenye ndoa zingine…” Kamene Goro alielezea.

Kamene alisema ukweli ni kwamba huku nje hakuna standards huku akiwataka watu kuchagua mtu ambaye anahisi kabisa wanalandana katika kile wanafanya.

“Acha nikwambie ukweli, huku nje hakuna standards, mimi nawaambieni, acha tutafute watu ambao wana maana katika maisha. Usiharibu muda wako kwa mtu ambaye hatakuja kuongeza thamani kwako. Mimi nisingekuwa na Bonez miaka hii yote kama hakuwa na kitu tunafanya. Sasa hivi tuko mwaka wetu wa tatu,” alifichua.

View Comments