In Summary

• Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Samidoh alipakia picha akiwa amesimama kando na gari na kuwashauri mashabiki wake.

Samidoh
Image: Facebook//Samidoh

Mwanamuziki wa Mugithi ambaye pia ni afisa wa polisi Samidoh ametoa ushauri wa kukanganya kwa mashabiki wake amabpo amezugumzia kuhusu kifo na jinsi mtu anavyopaswa kujiwekwa tayari kwa kile alisema kuwa kifo hakibishi hodi.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Samidoh alipakia picha akiwa amesimama kando na gari na kuwashauri mashabiki wake kwamba hakuja haja na kuweka pesa wakati hujui kifo kitabisha hodi muda gani, hivyo kuwataka kutumia pesa nyingi kwa manufaa ya miili yao na afya zao.

Lakini pia kwa usanjari huo, Samidoh alishauri kwamba unapotumia pesa zote uko nazo kwa mwili wako, usije ukasahu kuwa kuna uwezekano pia wa kuishi kwa miaka 90 kuelekea karne moja duniani, hivyo ni vyema pia ujali kesho yako kwa kuwekeza.

“Kifo kinaweza kuja wakati wowote kwa hivyo tumia pesa nzuri juu yako mwenyewe na ufurahie maisha. Usisahau pia kwamba unaweza kuishi hadi Miaka 90, jaribu na kuokoa pesa,” Samidoh aliwaacha mashabiki wake kwenye njia panda kwa ushauri huo wa kukata pande zote kama msumeno.

Baadhi walimuita kuwa mzungumzaji wa hadhara mwenye kutema madini ya busara, wakihusisha hali yake ya zogo baina ya babymamas wake ambalo limendelea kwa muda mrefu.

Mkewe Edday Nderitu yuko nchini Marekani kwa Zaidi ya mwezi mmoja sasa ambapo katika siku za hivi karibuni mwanasiasa Karena Nyamu ndiye ameonekana kuziba pengo hilo kwa kuonekana kila mahali na msanii huyo kama mume wake halali.

View Comments