In Summary

• Fina, mganga wa jadi maarufu, alisema hayo wakati wa onyesho lililomjadili mbunge mmoja wa zamani na aliyekuwa mjakazi wake aitwaye Joan Namatovu.

HISANI
Image: Vifaa vya uchawi.

Mganga wa jadi na mfanyibiashara maarufu nchini Uganda ambaye anafahamika na wengi kwa mujibu wa blogu za huko,  amezua gumzo mitandaoni baada ya kunukuliwa akisema kuwa yeye hawezi kuachwa tu kizembe zembe na mwanamume mpenzi wake.

Alisema kwamba mwanamume yoyote ambaye atampata na kumtangaza kama mume wake, basi moja kwa moja agano limefungwa na haliwezi kuvunjwa.

Na endapo mwanamume huyo atafanya mzaha wa kujaribu kuvunja uhusiano au kumtoroka, tafsiri yake itakuwa kwamba anatamani kifo kimkute.

"Mimi sipendezwi sana na wanaume," alisema mama huyo wakati akitokea kwenye runigna ya Sanyuka nchini humo, "kama napenda; sababu ya kuwakwepa [wanaume], ukinipenda na kunitoroka baadae, unakufa tu. Nadhani unajinyonga."

Mganga wa jadi maarufu, alisema hayo wakati wa onyesho lililomjadili mbunge mmoja wa zamani na aliyekuwa mjakazi wake aitwaye Joan Namatovu.

Namatovu aliajiriwa na mbunge huyo wa zamani na mwanahabari alipokuwa na umri wa miaka 17 mwaka wa 2005.

Uhusiano huo ulibadilika na kuwa uhusiano wa kimapenzi na hatimaye kuwa na mtoto naye, jarida moja linasimulia kisa hicho maarufu nchini Uganda.

Joan Namatovu aliweka hadharani suala hilo baada ya mbunge huyo kuwasilisha mahakamani kwa ajili ya kumlea mtoto wao wa kike mwenye umri wa miaka 10 mwaka wa 2021.

Wakati huo huo, kwenye show hiyo, Mganga huyo alionekana akiwa na mchungaji mmoja mtata.

Alimpa onyo la kufaya udhubutu: "Wewe si ujaribu [kunipenda]."

"Tunapaswa kuwaroga wanaume," Alitamka.

Mganga huyo wa kienyeji ni mwenye ushawishi mkubwa na mwenye uhusiano wa karibu na Rais Yoweri Museveni, anasemekana kumiliki biashara nyingi zenye mafanikio, hasa katika sekta ya usafiri na elimu, lilisema jarida moja.

 

View Comments