In Summary

• Kupitia Instastory yake, Diamond Jumapili jioni alipakia wimbo huo na kuonesha furaha yake kwa jinsi mashabiki wamempokea Lavalava.

Diamond amkumbuka Lavalava baada ya muda mrefu wa kumpotezea
Image: Facebook

Diamond Platnumz ni bosi mwenye furaha isiyo na kifani baada ya msanii wake wa muda mrefu aliyepoa na kunyamaa, Lavalava, kujiinua, kujikung’uta mavumbi na kujirudi tena kweney muziki.

Ikiwa ni karibia mwezi mmoja tangu Lavalava arejee na kibao cha Tajiri ambacho mtindo wake unakaa sana Amapiano, Diamond amekuwa mstari wa mbele kumsukuma Lavalava kwa kupakia wimbo huo kwenye akaunti zake kama njia moja ya kumpa promo kwa wafuasi wake Zaidi ya milioni 16 kwenye Instagram.

Diamond amefanay mwendelezo wa kupakia video na picha za jinsi wimbo huo unavyoendelea kufanya kwenye majukwaa mbalimbali haswa YouTube, ikiwa ni wiki moja tangu alipoiachia video yake.

Kupitia Instastory yake, Diamond Jumapili jioni alipakia wimbo huo na kuonesha furaha yake kwa jinsi mashabiki wamempokea Lavalava aliyekuwa kama amesahaulika kwenye lebo ya WCB Wasafi, ambapo alisema kuwa msanii wake ameamka kwa kasi ya 5G kwani alikuwa amenyamaa na kunyongonyea sana.

“Tulikaa kinyonge sana, Lavalava,” Diamond aliandika, akinukuu mstari mmoja kutoka kwa wimbo huo.

Tangu kuto kibao hicho, blogu na media mbali mbali zimekuwa zikimuangazia huku wengine wakimtania kwamba amefungua mdomo hatimaye, baada ya kusemekana kuingia gizani kwa Zaidi ya miaka miwili hadi akasahaulika kwamba bado yuko chini ya uongozi wa lebo hiyo inayotajwa kubwa kubwa Zaidi katika ukanda wa Afrika Masahriki kwa miziki ya kizazi kipya.

Awali kulikuwa na dhana mbalimbali kuhusu kupotea kwenye ramani ya muziki kwa Lavalava, baadhi wakizua kwamba alikuwa ametekwa nyara kwa mapenzi anayopewa na mpenzi wake mzungu, huku wengine wakidai kwamba ni uchawi ambao umetumwa Wasafi kiasi kwamba hata aimbe vipi bado hawezi kuonekana achia mbali kusikika.

Na ni vizuri pia ifahamike kwamba Lavalava si eti amekuwa bila kutoa miziki kwa kipindi hicho chote, la hasha! Msanii huyo amekuwa akiachia vibao vyako kadhaa lakini sema hvikuwahi kupata mapokezi makubwa kama ambavyo vilikuwa vinapokelewa awali – yani hata bosi wake mwenyewe hakufanya jitihada yoyote ya kusukuma kazi hizo zake na kuibua tetesi kwamba hakukuwa na maelewano mazuri baina yake na Lava.

View Comments