In Summary

• Waziri huyo alieleza kuwa ana hela mingi na akalinganisha pesa hizo kama kumwaga maji kwa bahari.

• Moses Kuria mnamo Juni 7, 2023, alimkashifu Eric Omondi katika mahojiano na runinga ya Citizen TV kuhusu ukosoaji wake wa kila mara kwa serikali.

Eric Omondi na waziri Moses Kuria.

Waziri wa viwanda na Biashara, Moses Kuria amepuuzilia mbali madai ya mchekeshaji Eric Omondi kwamba alimrejeshea shilingi 126,000 ambazo waziri huyo alikuwa ametumia kumpeleka Marekani.

Waziri huyo ambaye hapo awali alikuwa ameonyesha kusikitika kwake kwa kutumia pesa zake kumpeleka Eric katika ziara ya Marekani, alieleza kuwa ana hela mingi na akalinganisha pesa hizo kama kumwaga maji kwa bahari.

“Mwambie huwezi tuma maji kwa bahari. Waziri ako na pesa mingi huwezi rudisha. Sindio aliwaekea message fake. Imagine Eric Omondi atume Ksh26,000? Wacha Ksh126,000.” Alisema waziri huyo kupitia njia ya simu katika mahojiano na manablogu Eve Mungai..

Eric mnamo Juni 24, 2023, alishiriki picha ya M-Pesa inayodaiwa kuonyesha shilingi 126,000 zilizotumwa kwa waziri huyo.

Hata hivyo, wanamitandao waligundua kuwa hakuna neno 'M-Pesa' katika ujumbe alioshiriki Eric. Ujumbe wake ulisomeka 'Salio jipya la MPesa...' jina MPesa katika ujumbe huo ulikosa alama - .

Moses Kuria mnamo Juni 7, 2023, alimkashifu Eric Omondi katika mahojiano na runinga ya Citizen TV kuhusu ukosoaji wake wa kila mara kwa serikali.

Kuria alibainisha kuwa afadhali angetumia pesa hizo kujivinjari kuliko kumpeleka Eric katika ziara hiyo ya kwenda Marekani.

“Ni lazima tuwe watu ambao tunajilinganisha na dunia nzima. Nimeskia Eric akisema ni kijana. Miaka saba nilichukua pesa yangu nikampeleka America ndio aone dunia iko. Saa hii vile anaongea, afadhali ningetumia hio pesa kwa sherehe,” Kuria alisema huku akicheka.

Baada ya Kuria kumwaibisha kwenye runinga, Eric Omondi aliamua kuabiri ndege hadi London ili tu 'kula chakula cha mchana'.

“Baada ya kusikia Moses Kuria akizungumza, niliamua kujipeleka London kwa chakula cha mchana tu na pia namshukuru Mungu kwa umbali ambao ametufikisha,” Eric alisema kwenye video aliyopakia kwenye  InstaStory yake.

View Comments