In Summary
  • Alisema mwanamume asimtamani Mwanamke usiyeweza kumudu halafu unatuita Gold diggers, hata mkaa una thamani. Chagua mkaa wako na upike chakula chako ule ,msitupimie hewa "
Mwanamuziki na mfanyibiashara Akothee
Image: Instagram//Akothee

Msanii na mjasirimali maarufu Akothee ameeleza kuwa, mwanamke ni ua, usipolimwagilia litanyauka, ukilitia maji litastawi.

Akothee amewaambia wanaume wasivutiwe na wanawake wenye sura nzuri.

Kulingana naye, kutunza mwanamke mzuri hivi katika miaka yake ya 40 ni uwekezaji.

Alisema mwanamume asimtamani Mwanamke usiyeweza kumudu halafu unatuita Gold diggers, hata mkaa una thamani. Chagua mkaa wako na upike chakula chako ule ,msitupimie hewa "

Msanii huyo pia amewakashifu wanaume ambao wamekuwa na tabia ya kuwaita wanawake 'gold diggers'.

Akothee amewashsuri wanaume hao kuwatamani wanawake ambao wanaweza kuwadumu.

Mwanamke ni ua, usipomwagilia litanyauka, ukilitia maji litastawi. Usipende wanawake wenye sura nzuri, kushika mwanamke mzuri kiasi hiki katika miaka yake ya 40 ni uwekezaji sio nafuu 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Usifukuze Mwanamke usiyemudu halafu unatuita Gold diggers hata mkaa una thamani 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Chagua mkaa wako na upike chakula chako ule ,msitupimie hewa 🤣🤣🤣 Joka body Count 💃💃💃💃💃."

Haya hapa baadhi ya maoni ya mashabiki baada ya ujumbe wa Akothee;

munyualydia: Akothee umerudi kadem. You look amazing

mwikali: That is called the power of a substantial body count

anita: The fact that you walk so effortlessly in heels at your 40's na Mimi Niko in my 20's na heels zimenishinda

ifakaracakes: Mie charcoal nimekaa kwa kutuli❤️❤️😂😂

pidzo: So akoth is cute🤔ama ni mimi niko jaba😂

lemiso: 😂😂😂borake Mimi niwatch hii video bila sauti

 

View Comments