In Summary

• Daddy owen alieleza sababu kuu ya kufungua kituo chake cha Care kilitokana na mapenzi yake ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu na wazazi wao.

• Daddy Owen alizungumza haya akiwa anajibu maswali ya wafuasi wake baada ya kukosa kuchapisha picha za mtoto wake alipokuwa akishereheka siku ya kuzaliwa ya mwanawe.

Daddy Owen Daddy Owen aeleza sababu ya kufungua kituo cha kuwasaidi awatoto walemavu.
Image: INSTAGRAM// DADDY OWEN

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Daddy Owen amelezea sababu ya kuanzisha kituo cha kutoa huduma watoto walemavu pamoja na wazazi wao.

Akizungumza na mwandishi mmoja wa Radio Jambo, Daddy owen alieleza sababu kuu ya kufungua kituo chake chaCare kilitokana na mapenzi yake ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu na wazazi wao.

"Kuna hospitali hapo Kijabe inaitwa Cure Kenya, Mimi hutembea kaunti zote nchini kutafuta watoto wenye ulemavu na sasa ukitaka kuwachukua watoto hawa kuwapeleka hopitali hio lazima umlete na mzazi ili mzazi afahamu pahali unapeleka mtoto wake."

Aliongeza: "Vitanda vya hospitali ya Cure ni vidogo kwa hivyo haviwezi kuwatosha wazazi na watoto wao, hata mzazi hawezi achilia mtoto wake atoke na hajui anaenda wapi, sasa unawaleta wote na wazazi ili mtoto ajihisi nyumbani karibu na wazazi wake.”

Daddy Owen alizungumza haya akiwa anajibu maswali ya wafuasi wake baada ya kukosa kuchapisha picha za mtoto wake alipokuwa akishereheka siku ya kuzaliwa ya mwanawe.

Daddy Owen alisema alihisi haikuwa sawa kuchapisha picha za mwana wake kwa sababu hakutaka watu wamfahamu mwanake bila hiari yake. Aliilinganisha kisa hicho na mwanasoka na mkufunzi wa timu ya Real Madrid Zinadine Zidane kufichua mtoto wake na kusabibisha kupata shinikizo la kufikia kiwango cha baba yake katika ulingo wa soka.

"Nikama watoto wa wachezaji soka wanataka kuwa kama wazazi wao na kuazimia kufikia kiwango cha mzazi wake. Mfano mzuri ni Zinadine Zidane. Zidane alikuwa mchezaji mzuri sana alafu akukuwa mkufunzi, wakati huo akamfanya mwanawe ajiunge na timu ya Real Madrid na mtoto huyo hakufanya vyema."

Daddy Owen alionekana kuwashauri watu maarufu kukosa kuwatambulisha watoto wao kwa umma kwa sababu si kila mtu angependa kuwa maarufu. Kulingana na Owen chaguo hilo linaweza kuathiri matokea ya shule ya watoto hao.

View Comments