In Summary

• Mzee huyo alirejea kwenye klabu hiyo ambayo ilikuwa inafunguliwa tena baada ya miaka 10.

• Alipelekwa kweney klabu hiyo na mwanamke ambaye anamlea katika uzee wake.

Kevin Topham Mkongwe wa miaka 95 aliyerejea kwenye klabu alikompata mkewe mwaka 1949.
Image: BBC NEWS

Kulishuhudiwa kioja cha kuzuzua nyoyo baada ya mzee mwenye umri wa miaka 95 ambaye ni mkongwe wa jeshi la angani la Uingereza kujitosa kwenye jukwaa la densi katika hafla ya ufunguzi upya wa klabu ambako alimpata mke wake kwa mara ya kwanza miaka 74 iliyopita.

Kwa mujibu wa Daily Mail, Kevin Topham, kutoka Edingley, Nottinghamshire, alimtazama kwa mara ya kwanza mke wake mtarajiwa Molly mnamo 1949 kwenye Corn Exchange huko Newark - ambayo sasa imefunguliwa upya ikiwa na jina Club X.

Wawili hao walifunga pingu za maisha miaka mitatu baadaye na walioa kwa miaka 66 hadi Moly alipoaga dunia mwaka wa 2018.

Katika miaka ya hivi majuzi, Donna Harvey - ambaye ni mlezi wa Kevin - alielezea jinsi mkongwe huyo angekumbuka kumbukumbu zake za furaha klabuni kila walipopita kwa gari kwenda kwa miadi ya daktari au kutembelea familia.

Baada ya kugundua kuwa klabu hiyo ilikuwa ikifunguliwa tena kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10, Donna aliiambia BBC News jinsi alivyowauliza wamiliki kama angemletea Kevin kwa densi usiku wa ufunguzi.

Hapo awali, Donna alisema alijaribu kumwonya Kevin kwamba klabu haitafanana na jinsi alivyoikumbuka - lakini alisisitiza kujionea mwenyewe.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Donna na Kevin walikuwa wageni wa kwanza kwenda kwenye sakafu ya ngoma usiku wa ufunguzi.

Akielezea jinsi alivyohisi 'kuhisi hisia kidogo' kuwa katika klabu hiyo tena, Kevin alisema wafanyikazi wapya walimfanya ahisi 'kukaribishwa sana'.

Zaidi ya hayo, mstaafu huyo alitania kwamba mara kwa mara angepata wapenzi watatu watarajiwa kwenye sakafu ya densi miaka ya 1940s - na wakati fulani ilimbidi kurusha sarafu ili kumchagua mmoja anayemfaa.

View Comments