In Summary

• Tyga alichapisha picha za matatu ya kijani kwenye barabara ya Kenya ambayo ilikuwa na picha yake na jina lake.

•Kuona upendo mwingi alioonyeshwa na mashabiki Wakenya, rapa huyo wa Marekani aliapa kufanya ziara katika siku za usoni.

Tyga
Image: HISANI

Rapa wa Marekani Micheal Ray Stevenson almaarufu Tyga ameshangazwa na baadhi ya matatu za Kenya kuwa na michoro yake ya graffiti.

Siku ya Alhamisi, Tyga alichapisha picha za matatu ya kijani kwenye barabara ya Kenya ambayo ilikuwa na picha yake na jina lake.

"Hii iko wapi ulimwenguni na iko na nini?" Tyga aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.

Shabiki mmoja alimjibu akimjulisha kuwa matatu hiyo ilikuwa mjini Mombasa na pia akamfahamisha kuhusu magari mengine zaidi yenye picha zake jijini Nairobi.

"Lazima iwe Mombasa Kenya.. lakini hata tuna zaidi Nairobi Kenya," @mudryk254 alimwambia mwimbaji huyo wa nyimbo za kufoka na kuambatanisha ujumbe wake na picha za matatu zilizochorwa picha na jina lake.

Kuona upendo mwingi alioonyeshwa na mashabiki Wakenya, rapa huyo wa Marekani aliapa kufanya ziara katika siku za usoni.

"Oh, ni lazima nifanye ziara siku moja," alisema.

Alibainisha kuwa alikuwa amependa kutambuliwa na upendo aliokuwa akipata kutoka kwa mashabiki wa Kenya.

Tyga ni rapper wa Marekani mwenye umri wa miaka 33 ambaye alisaini mkataba wa kurekodi na Young Money Entertainment, Cash Money Records na Republic Records mwaka 2008 baada ya kufanya nyimbo kadhaa pekee.

Anajulikana kwa nyimbo zake maarufu kama vile Ayo, Loco Contigo, Taste, Bored in The House miongoni mwa zingine.

View Comments