In Summary

•Raburu aliondoka Royal Media mwezi uliopita baada ya miaka 13, akiwaacha mashabiki wake wengi wakiwa wamevunjika moyo.

•"Niligundua kuwa sijawahi kupumzika, nilihitaji kupumzika. Nilitaka tu kufanya kitu kipya, na kupumzika," Raburu alisema.

Willis Raburu katika studio za Radio Jambo
Image: RADIO JAMBO

Mwanahabari Willis Raburu amefunguka kuhusu ni kwa nini aliacha kazi yake nzuri katika runinga ya Citizen.

Raburu aliondoka Royal Media mwezi uliopita baada ya miaka 13, akiwaacha mashabiki wake wengi wakiwa wamevunjika moyo.

Katika mahojiano na Mark Masai, alisema alikaa miaka hiyo yote kwa sababu alipenda mazingira ya kazi katika Royal Media.

"Nilikuwa mwaminifu kwa Royal. Ilikuwa utamaduni wa shirika.

Wenzangu walikuwa wazuri na nilipenda jinsi kampuni ilivyofanya kazi na sera yao ya mlango wazi.

Katika kipindi ambacho nimekuwa huko, nilifanya mambo tofauti kati ya hadithi za migogoro, kisiasa, maslahi ya kibinadamu

Nilianza kufanya ushauri wa kidijitali kwa makampuni.

Niligundua kuwa sijawahi kupumzika, nilihitaji kupumzika. Nilitaka tu kufanya kitu kipya, na kupumzika.

Ninakaribia kumaliza Shahada yangu ya Uzamili katika USIU na hiyo ilinifanya kupanua mawazo yangu." alisema.

Raburu anasema kwa muda mrefu alikuwa akitaka kuwa mwanahabari.

"Nilikuwa nimewaambia mama yangu na shangazi kwamba nitasoma habari kwa kuwa ndicho kitu pekee kilichomfanya baba yangu 'kunyamaza.' licha ya jinsi alivyokuwa na nguvu wakati huo."

Raburu anasema angekosa hafla za familia kutokana na aina ya kazi yake hadi watu wakaacha kumwalika.

Sasa anasema anaweza kuzingatia kuwa na muda zaidi na familia.

View Comments