In Summary

• Mulamwah alibainisha kuwa yeye hakuhisi ikiwa sawa kuishi katika jumba kubwa kwa sasa kwani hana familia kubwa

• Alifichua kuwa yeye hulipa kodi yake mwanzo mwaka na kuishi bila wasiwasi wa kuitishwa kodi hiyo na mwenye nyumba.

Mulamwah.
Image: Facebook

Mmoja wa wacheshaji maarufu Mulamwah, hatimaye amejitokeza na kufichulia umma sababu ya yeye kuishi kwenye bedsitter licha ya kujitokeza hadharani na kutangaza alikuwa milionea.

Akizungumza kwenye Kutit Podcast, Mulamwah alibainisha kuwa yeye haoni ikiwa sawa kuishi katika jumba kubwa kwa sasa kwani hana familia kubwa kwa hivyo anajihisi akiwa na starehe akiishi katika chumba hicho kimoja.

"Kwa sasa mimi sifeel kama nahitaji kuishi kwa nyumba kubwa. Unaeza kuwa unaishi kwa bedsitter lakini hii ni Iphone 14 niko nayo hapa. Nilinunua hii simu kwa sababu ninaitumia kufanya kazi yangu hapa na hata ingekuwa milioni moja bado ningeinunua. Sihitaji nyumba kubwa sai na niko peke yangu," alieleza Mulamwah

Mchekeshaji huyo alifichua kuwa yeye hulipa kodi yake mwanzo wa mwaka na kuishi bila wasiwasi wa kuitishwa kodi na mwenye nyumba.

Mulamwah alieleza sababu ingine inayomfanya atumie fedha kidogo kwenye kodi ya nyumba ni kutokana na kwamba kwa sasa anajenga jumba la kifahari kijijini kwake.

Mulamwah amechapisha picha zake akiwa ndani ya nyumba yake kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii mara kadhaa. Watu wengi waliona ni kwamba nyumba yake daima haina mpangilio.

Mcheshi huyo alisema kuwa sababu ya nyumba yake kuwa haikuwa na mpangilio na anaonekana nadhifu, ni mpangilio tu ili aweze kuunda maudhui. Yeye huwa anaifanya ionekane haina mpangilio, ili watu waelewe zaidi.

Alisema katika uundaji wa maudhui ili mtu aweze kuvuta hisia za hadhira, ni lazima atumie mifano ambayo hadhira inaweza kujihusiha na kuhisi inawaguza kibinafsi.

View Comments