In Summary

• Mwangi ambaye alikuwa mwanahabari mpiga picha alibadili nia yake baada ya kushuhudia machafuko yaliyojiri katika uchaguzi wa mwaka 2007.

Boniface Mwangi asherehekea kufikisha miaka 40.
Image: Facebook

Mpiga picha aliyegeuka mwanaharakati wa kupigania na kutetea haki za kibinadamu Boniface Mwangu anafikisha umri wa miaka 40 leo hii Jumatatu na katika ujumbe wake, ameweka wazi kwamab hana ndoto ya kuacha uanaharakati muda wowote hivi karibuni.

Mwangi kupitia kurasa zake mitandaoni alipakia picha mbili – moja ikiwa ya utotoni na nyingine ya ukubwani na kusema kuwa ndoto yake ni kuendelea kuomba Zaidi, kuwa baba bora kwa wanawe bila kusahau kuendelea kupigania Kenya iliyo bora hadi ile siku ambayo Mungu atampumzisha kutoka duniani.

Mwanaharakati huyo asiye na woga aliwashukuru watu wa karibu na yeye ambao kila siku wamekuwa wakimpa himizo la kusimama na kupigania kile anahisi ni bora kwa Kenya bila kujali madhara ambayo huambatana na uanaharakati wa namna hiyo.

“Leo ninatimiza miaka 40. Haijakuwa rahisi ikiwa haikuwa kwa Mungu na mfumo wangu wa usaidizi mwaminifu. Kwa familia yangu na marafiki, ambao wamekuwa daima kwa ajili yangu, niko hapa leo kwa sababu yako. Asante kwa upendo na msaada wako,” Mwangi alisema.

“Najiahidi kuomba zaidi, mzazi bora, niendeleze mapambano mazuri ya Kenya iliyo bora, na kuwa na wakati mzuri hadi siku Mungu atakaponiita nyumbani,” aliongeza.

Mwangi ambaye alikuwa mwanahabari mpiga picha alibadili nia yake baada ya kushuhudia machafuko yaliyojiri wakati wa vurugu za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007-08.

Baadae mwaka 2008, alitumia picha hizo na kuanza kuzionesha waziwazi akipinga vikali jinsi ambavyo watu walikuwa wanauana kwa kukatana kwa panga.

Tangia hapo, amekuwa katika mstari wa mbele kupigania haki za kibinadamu, haswa katika mstari wa wanasiasa ambao wanachagiza baadhi ya vitendo visivyofurahisha nchini.

View Comments