In Summary

• Alikiba alikuwa na mkusanyiko wa wasanii wengine akiwemo meneja wake pamoja na msanii Marioo.

Diamond Platnumz, Al8ikiba
Image: INSTAGRAM

Wasanii wengi wa Bongo Fleva wameimezea mate sana mwezi huu wa Julai wakisema kuwa ndio mwezi wa kurudi upya kwenye muziki baada ya kupoa kwa muda.

Iianza na msanii Diamond Platnumz kutangaza kwamba mwezi Julai ndio atafanya urejeo upya kwa muziki na hata kutamba kwamba atashikilia chati kwenye trend namba moja hadi Janauri mwakani atakapochukua likizo fupi kumpisha msanii wake mpya.

Baada ya kutaja kuwa analenga kuteka trends zote za muziki, Alikiba alitoa tamko ambalo limetajwa kuwa mshale kwa kambi ya Diamond Platnumz akisema kuwa yeye hutoa miziki mikali na wala hajali mambo na trends.

Alikiba alikuwa na mkusanyiko wa wasanii wengine akiwemo meneja wake pamoja na msanii Marioo.

Katika maongezi yao ilionekana Marioo na Alikiba walikuwa wanatoa collabo na Marioo alisema kuwa noma hiyo isipohit basi ako radhi kumpa meneja wa Alikiba shilingi milioni 50 za Kitanzania.

Hapo ndipo ALikiba alidamka na kutia neno akisema kuwa;

“Nyinyi mnajali kuhusu trends,” Alikiba alisema.

Kauli hii ilipokelewa kwa njia tofauti na mashabiki wa muziki wa Bongo Flava baadhi wakisema kuwa kauli hiyo ilikuwa inalenga kwa Diamond baada ya kusema kuwa atakuwa anashikilia namba moja kwenye trends.

Kwenye sehemu ya komenti ilikopakiwa hiyo video, walionekana wakiotesha ugomvi wa wasanii hao wawili, licha ya Diamond mara nyingi tu kukanisha hadharani kwamba yeye na Kiba hamna uadui baina yao bali ni vyombo vya habari na mashabiki ambao wamekuwa wakiwapiganisha bure.

 

View Comments