In Summary

• Diana Marua amejitokeza na kuonyesha kughadhabishwa kwake na video zilizokuwa zikisambaa mitandaoni ya mpenzi wake akimvisha mwanamke nguo yake.

• Hivi majuzi bahati alimchumbia rasmi mpenzi wake wa muda mrefu na mzazi mwenzake Diana Marua. 

Mwanasoshalaiti Diana Marua amejitokeza na kuonyesha kughathbishwa kwake na video zilizokuwa zikisambaa mitandaoni ya mpenzi wake akimvisha mwanamke nguo yake.

Diana akipeleka malalamishi yake kwenye akaunti yake ya Instagram, alieleza kuwa hakutaka kutazama video hiyo na kuongeza koti ambayo Bahati alimpa mwanamke huyo aliinunua mwenyewe.

"Heeeeeee!!! Sijataka kuiskiza na sauti halafu ndio imeuma zaidi. Lakini , si hiyo jacket nilikununulia aki??? wanaume watakuacha kwenye jangwa bila???" Diana aliwaacha wafuasi wake kujijazia hilo.

Bahati aliibua gumzo mitandaoni baada ya kunengua viuno na mrembo mmoja alipokuwa akitumbuiza katika klabu mmoja mjini Kitale.

Bahati akionekana kufurahia muda na mwanamke huyo ambaye bado hajafahamika alitoa koti aliyokuwa amevaa na kumvisha mwanamke huyo kwa njia iitowafanya watu kuhisi kulikuwa na zaidi ya kudensi tu.

Baada ya tukio hilo Bahati alilazimika kumuomba msamaha hadharani mchumba wake kwa kumpikia chajio.

"Finally nimerejea nyumbani kwa mke wangu na njia pekee ya kuomba msamaha kwa kile nilichofanya ni kuelekea moja kwa moja na kupika dinner... aki mapenzi wewe ata hakuna kupumzika."

Hivi majuzi Bahati alimchumbia rasmi mpenzi wake wa muda mrefu na mzazi mwenzake Diana Marua. 

Wakati akichukua hatua hiyo kubwa, Bahati alibainisha kuwa amekamilisha hatua zote muhimu kuelekea ndoa na sasa yuko tayari kuifanya rasmi.

"Umenipatia moyo wako. Kusema kweli kutoka ndani ya moyo wangu, siichukulii virahisi. Kitu kimoja ambacho ninataka sana kufanya mwaka huu, nataka tu kuhakikisha nimefanya sawa, najua nimeenda kwa familia yako kwa utambulisho lakini mwaka huu nataka tufanye harusi ya kweli na nataka kukuoa,"  Bahati alimwambia mchumba wake.

View Comments