In Summary

• "Kwenye imefikia sasa hivi ni pale penye ninaweza amua nimalizie vyumba viwili kwanza nikae nikiendelea kujipanga" - Mulamwah.

Mulamwah azunguzia maendeleo ya ujenzi wa jumba lake la kifahari.
Image: Facebook

Mwaka jana mchekeshaji Mulamwah alitangaza kwa furaha kwa wafuasi wake mitandaoni uzinduzi wa mradi wake mkubwa kijijini kwao ambao ulikuwa ni ujenzi wa jumba lake la kifahari.

Kwa muda, mchekeshaji huyo amekuwa akiwaonyesha mashabiki wake safari ya hatua mbalimbali za mjengo huo kutoka uchimbaji msingi hadi kusimamisha nguzo, na sasa amesema kwamba mpaka hatua ambayo amefikia katika ujenzo huo, tayari ametumia kiasi cha shilingi za Kenya milioni 7.

Mulamwah alimwambia Mungai Eve kwamba mjengo huo uko mbali sana na kukamilika kwani ndio mwanzo amepita nusu kiasi tu katika ujenzi.

Mulamwah alisema kuwa mchakato mzima umempa funzo kubwa ambapo amejipata kubanwa kiasi kwamba hawezi fanya jambo lolote la ziada.

“Ni kitu poa naweza sema ni mchakato mzuri ambao umakufungua akili, huwezi poteza hata senti. Hata suruali huwezi ongeza kusema kweli. Simiti haichezi na chuma. Penye imefika sasa hivi tunafanya fabrication kuweka madirisha, milango na vitu vingine. Hiyo kitu ni noma. Sikujua ni noma hivo,” Mulamwah alielezea uzoefu wake.

“Sasa hivi nimetumia kama milioni 7 na ndio tumepita tu nusu kiasi, yaani sikuwa najua inaweza kuwa noma hivyo. Ni mradi mzuri ambao una ahadi ya siku za usoni. Kwenye imefikia sasa hivi ni pale penye ninaweza amua nimalizie vyumba viwili kwanza nikae nikiendelea kujipanga,” aliongeza.

Mchekeshaji huyo alisema kuwa kulingana na makadirio ya bajeti ambayo alipatiwa na mafundi mwanzoni akianzisha ujenzi, mradi mzima hadi kukamilika utatumia hadi shilingi milioni 11.

“Haina mbio, hakuna makataa na si eti ni kitu yenye ninataka kulala hapo kesho keshokutwa. Ni pole pole tu kulingana na mfuko na jinsi uchumi wa Kenya unayokua,” alisema.

View Comments