In Summary

• Na safari hii ameubuka katika wajibu huo kwenye wimbo wa Ova amabo umetungwa na msanii wa Nigeria, Lojay.

TANASHA DONNA ashiriki kwenye ngoma ya msanii wa Nigeria kama Vixen wa Video.
Image: Screengrab//YouTube

Mtangazaji na mwanamuziki Tanasha Donna amerejea kule alikoanzia enzi anakwea kwenye ngazi za kutafuta umaarufu miaka michache nyuma.

Msanii huyo baada ya kimya cha muda, hatimaye ameibuka, na safari hii ni katika video ya wimbo wa msanii wa Nigeria ambapo hajashirikishwa kama mwimbaji bali ameshiriki kama video vixen.

Itakumbukwa kwamba Donna alianza kufahamika na wengi katika wajibu wake wa video vixen aliposiriki kwenye video ya wimbo wa Alikiba aliomshirikisha Christian Bella, Nagharamia miaka takribani kumi iliyopita.

Na safari hii ameubuka katika wajibu huo kwenye wimbo wa Ova amabo umetungwa na msanii wa Nigeria, Lojay.

Wimbo huo kwa mbali una maudhui ya kuvunja uhusiano wa kimapenzi na Donna katika ustadi wake aliweza kuvaa wajibu wake vizuri kabisa ambapo anaigiza japo katika baadhi ya scenes wanaonekana kama wanaoangaliana kwa mahaba mazito machoni mwao nusura kupatiana busu.

Mama huyo wa mtoto mmoja amekuwa akihusishwa kuwa na mpenzi kutoka nchini Nigeria mara kadhaa ikiwa ni miaka kama minne hivi tangu kuachana na baba wa mtoto wake, msanii Diamond pLatnumz kutoka Tanzania.

Lakini katika safari zote hizo, Donna amekuwa akikanusha vikali kuwa na mpenzi kutoka Nigeria huku akiwa msiri sana katika maisha yake ya kimapenzi tangu kuachana na Diamond – kiasi kwamba hakuna anayejua iwapo anachumbiana tena au la.

View Comments