In Summary

• Niko singo kwa sababu kila muda ninapowekeza hisia zangu kwa mtu, wananionesha hakika kwa nini niko bora nikiwa peke yangu - Diamond.

DIAMOND PLATNUMZ Asimulia kwa mfadhaiko sababu za kukosa mpenzi
Image: Screengrab//YouTube

Msanii namba moja wa muda wote katika muziki wa Bongo Flava, Diamond Platnumz kwa mara nyingine amerejelea suala la yeye kukosa kuwa na mwanamke yeyote kimapenzi licha ya kubarikiwa kwa kila kitu.

Katika video fupi ambayo ameipakia kwenye Instastory zake, Diamond alieleza sababu zake za kufanya uamuzi wa kuwa bila mpenzi, akisema kuwa hajafanya uamuzi huo kwa kukosa mtu wa kuwa naye bali ni uamuzi wak ulinda moyo wake dhidi ya mfadhaiko lakini pia kuzingatia Zaidi katika Sanaa yake ya muziki.

Kwenye video hiyo ambayo ni ya mtu aliyekuwa anatoa sababu za kuwa singo, Diamond alihisi ujumbe huo unamfaa katika hali yake ya sasa hivi na kuitumia kuelezea yaliyoko moyoni mwake na akilini mwake vilevile.

Kinadharia, Diamond alikuwa na maana kwamba amechagua kuwa bila mpenzi kwa sababu amejaribu siku za nyuma kuwekeza hisia zake kwa mtu lakini mtu huyo akamalizia kumkwaza na hivyo kuwaza kwamba pengine yeye ni bora Zaidi wakati ako peke yake.

“Siko singo kwa sababu siwezi pata mtu. Niko singo kwa sababu kila muda ninapowekeza hisia zangu kwa mtu, wananionesha hakika kwa nini niko bora nikiwa peke yangu,” Video hiyo ilisema.

Msanii huyo alipakia video hii ikiwa ni siku chache tu baada ya kufahamika kwamba aliyekuwa mke wake na ambaye sasa ni mzazi mwenziwe, Tanasha Donna kutoka Kenya amerejea katika taaluma ambayo ilimpa umaarufu miaka michache iliyopita – kucheza kama video vixen.

Donna kupitia Instagram yake aliweka wazi kwamba ameshiriki kama vixen wa video katika wimbo wa msanii kutoka Nigeria, Lojay.

Ikumbukwe Donna alifahamika na wengi baada ya kushiriki kama vixen wa video kwenye wimbo wa Alikiba aliomshirikisha Christian Bella kwa jina Nagharamia miaka 7 iliyopita.

View Comments