In Summary

• Bahati alisema, "Ndiyo sote tuna haki ya kujieleza lakini tusitumie fursa hiyo kupigana sisi kwa sisi, tusiitumie kumwaga damu, tusiitumie kuharibu mali ya masikini mwenzako kwa jina la Maandamano."

• Aliongeza kuwa Rwanda ilipoteza Zaidi ya Watu Milioni 1 katika Siku zisizozidi mia moja kwa sababu ya Ukabila na Uchochezi wa Kisiasa.

Kevin Bahati anawashauri Wakenya kutoruhusu siasa kuwagawanya.
Image: Instagram

Msanii Kevin Bahati anawashauri Wakenya kutoruhusu siasa kuwagawanya kwani, hakuna mwanasiasa hata mmoja anayeweza kufa kwa ajili ya mwananchi hivyo basi anawashauri wananchi kutokubali kufa kwa ajili yao.

Alisema kuwa kutokana na kutazama habari kwenye maandamano alijihisi kusema kuwa iwapo vita vya wenyewe kwa wenyewe baina ya wananchi vikianza siku hiyo basi, Wanasiasa watachukua ndege ya kwanza na kukimbilia majuu.

"HAKUNA MWANASIASA MMOJA anayeweza kufa kwa ajili yako hivyo hupaswi kufa kwa ajili yao! Na Vita vya wenyewe kwa wenyewe Vikianza Leo Kenya Wanasiasa hawa Wataabiri Ndege ya Kwanza Wakimbilie Majuu... Huyo Mama Mboga unayemuibia ndio utakopa Sukuma Kwake Economy ikiumana," aliandika msanii huyo.

Msanii huyo aliendelea kwa kuelezea wananchi kuwa wajifunze kutoka kwa yale yaliyowapata wakati wa vurugu baada ya Uchunguzi wa 2007.

"Ndiyo sote tuna haki ya kujieleza lakini tusitumie fursa hiyo kupigana sisi kwa sisi, tusiitumie kumwaga damu, tusiitumie. kuharibu mali ya masikini mwenzako kwa jina la Maandamano," alisema kwa huzuni.

Bahati alisema kuwa kutembelea makaburi ya halaiki na kusikiliza Hadithi za jinsi Damu ilivyomwagika na Mali Kuharibiwa ni moja ya Nyakati zake ngumu sana nchini Rwanda.

Aliongeza kuwa Rwanda ilipoteza Zaidi ya Watu Milioni 1 katika Siku zisizozidi mia moja kwa sababu ya Ukabila na Uchochezi wa Kisiasa.

"Naziombea Nguvu Familia zote zilizopoteza Wapendwa wao Leo na Vijana Wenzangu Wanaotumika katika Maandamano haya; Mungu Akulinde unapojaribu kuifanya kwa njia ya Amani kwa mujibu wa Sheria bila Kuharibu Mali ya Jirani 🙏.

Sisi ni Viongozi wa Kesho... kwa hivyo tukiwapiga vijana wetu kwa risasi za bunduki Leo Ni wazi hakuna Kesho! Amani na Umoja viwepo kwa Jina la Yesu 🙏 NAKUPENDA MAMA YANGU NCHI KENYA 🇰🇪," aliandika msanii huyo.

View Comments