In Summary

• Video hiyo ilizoenekana na meza ya Radio Jambo, ilimwaonyesha Shakilla akiwa amemlalia  mwanamuziki huyo kifuani bila nguo ila chupi tu huku LavaLava akiwa kwenye usingizi mzito

• Shakilla hata hivyo amejitokeza na kuelezea kuwa video hiyo si ya hivi majuzi na ameshangaa kuiona video hiyo mitandaoni baada ya tukio hilo kufanyika miaka miwili ilyopita.

Mwanasosholaiti Shakila
Image: Shakila (Instagram)

Mwanasosholaiti maarufu Shakila ameonekana katika video zinazoenea mitandaoni akiwa na mwimbaji wa nyimbo za Bongo Fleva, LavaLava.

Video hiyo ilizoenekana na meza ya Radio Jambo, ilimwaonyesha Shakilla akiwa amemlalia  mwanamuziki huyo kifuani bila nguo ila chupi tu huku LavaLava akiwa kwenye usingizi mzito.

Wanamtandao hawakupoteza wakati kuchangia mawazo yao kuhusu video hiyo ambayo haijabainika ni ya lini. Mmoja kati ya wanamitandao alisema kwa ucheshi, "Ogopa usingizi baada ya mechi."

Shakilla hata hivyo amejitokeza na kuelezea kuwa video hiyo si ya hivi majuzi na ameshangaa kuiona video hiyo mitandaoni baada ya tukio hilo kufanyika miaka miwili ilyopita.

"Kuna video yangu na mtu mnayemfahamu inayosambaa mitandaoni, ningependa mfahamu pia mimi ninmeshangazwa kuona video hiyo kwa sababu video hiyo ilirekodiwa zaidi ya miaka miwili iliyopita." alieleza Shakilla.

Soshalaiti huyo alibainisha kuwa video hiyo ilirekodiwa kwa simu ya mtu ambaye hakumtyambulisha na kuongza kuwa hawajakuwa kwenye mawasiliano na mtu huyo kwa zaidi ya mwaka mzima.

Shakilla mwenye umri wa miaka 22 alisema hatazungumzia video hiyo tena na si yeye aliyechapisha video hiyo.

Shakilla awali alikuwa ameibua tetesi kuwa walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki kutoka nchi ya Nigeria Omah Lay baada ya kuchapisha picha katika Instastory yake wakiwa na mwanamuziki huyo.

Shakila awali alijitokeza kimasomaso na kukiri kuwaa hawezi akajihusisha katika mahusiano na mwanume kutoka Kenya.

“Siwezi kuchumbiana na Mkenya kamwe. Mimi si Mkenya kwa hivyo nina haki ya kufanya hivyo."

Kulingana naye angependelea kuchumbiana na wanaume wa Nigeria, ambao aliwasifu kwa ukarimu wao.

"Wanigeria ndio watu watamu zaidi unaoweza kukutana nao, wanakupa pesa na kukutendea mema.

View Comments