In Summary

• Kwa kawaida, madaktari wanashauri akina mama wanaonyonyesha kuepuka kunywa kwa kipindi ambacho wananyonyesha watoto wao wachanga kwani inaweza kuathiri maziwa yao.

• Mwanafasheni huyo wa mitandaoni, ambaye alimkaribisha bintiye miezi miwili iliyopita, alifichua kuwa alianza kunywa pombe baada ya kupata ruhusa kutoka kwa daktari.

Amber Ray alia kukosa maziwa ya kunyonyesha mtoto wake.
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Amber Ray amejibu shutuma kutoka kwa watu waliomhoji kwa nini anakunywa pombe ila alitakiwa kunyonyesha.

Kwa kawaida, madaktari wanashauri akina mama wanaonyonyesha kuepuka kunywa kwa kipindi ambacho wananyonyesha watoto wao wachanga kwani inaweza kuathiri maziwa yao.

Mwanafasheni huyo wa mitandaoni, ambaye alimkaribisha bintiye miezi miwili iliyopita, alifichua kuwa alianza kunywa pombe baada ya kupata ruhusa kutoka kwa daktari.

"Najua hufai kunywa pombe mpaka mtoto afikishe miezi sita kwa wale wanaonyonyesha. Nilijaribu kumnyonyesha mtoto wangu, sasa ana miezi miwili lakini maziwa yalikataa kabisa.

Nilijaribu kila kitu. Nilitaka kunyonyesha lakini ilikataa kabisa. Basi daktari akaniambia kama imekataa imekataa, na sinyonyeshi ndiyo maana naweza kunywa (najua hutakiwi kunywa hadi baada ya miezi sita...lakini maziwa yangu yalikataa, daktari akaniambia kama siwezi kunyonyesha basi siwezi kunyonyesha. , ndiyo maana ninakunywa)," alisema.

Video hiyo iliyopakiwa kwenye Tiktok iliwaacha watumiaji wa mitandao ya kijamii na maoni tofauti, huku wengine wakijiuliza ikiwa hiyo ilitokana na hali ya kiafya au kulingana na mtindo wake wa maisha.

"Aaaiiii alikula njahi, uji, drinking chocolate, chapati ya brown?" Anasteh Kihara aliuliza.

"Celebs hawananga maziwa sijui ni kwa nini," Lucy Njoki737 aliandika.

"Ni ukweli hadi mimi nilijaribu kila kitu lakini ilikataa," alisema Zamzam Sumey.

"Hapa pia,,,maziwa ilikataa ilinisumbua sana ikabidi niende kuchukua maziwa ya Nan," Catenzilani1595 alisema.

"YOU OWE NOBODY AN EXPLANATION!...muache maisha ya watu!" Kiddo_mumbi alisema kwa mbwembwe.

"Nilijifungua kwa kupitia cs na maziwa ilikosa kabisa. Isitoshe nilijaribu kila kitu lakini wapi," Maureen alisema.

"Itakuwaje wanasosholaiti wote hukataa?? Hildahmwihaki625 aliuliza.

Wiki chache zilizopita Amber alisema kuwa wakati alikuwa akimnyonyesha mtoto wake wa kwanza, Gavin miaka 13 iliyopita, alikuwa na maziwa ya kutosha na alikuwa anatarajia hivyo kwa bintiye Africana, lakini amepigwa na butwaa kugundua hana maziwa ya kutosha.

Mwanasosholaiti huyo ambaye amekuwa akionekana mitandaoni licha ya kuwa mama mwenye mtoto mchanga alitania kuwa pengine ni kutokana na mtoto huyo mdogo kuwa wa tajiri, akiibua dhana kuwa pengine watoto wa matajiri huwa hawapendi maziwa ya mama.

Amber Ray alia kukosa maziwa ya kunyonyesha mtoto wake.
Image: Instagram
View Comments