In Summary

•Kando na usanii, mwimbaji huyo pia amekuwa katika mstari wa mbele kuzipigania haki za kibinadamu hasa watoto walemavu.

Daddy Owen
Image: INSTAGRAM// DADDY OWEN

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Daddy Owen amekiri kuwa hataacha kuziimba nyimbo za injili kamwe hata iwe nini.

Katika mahojiano Alhamisi 13, Owen ameeleza kuwa yeye aliitwa na kuupokea wito wa kutangaza injili kabla ya uimbaji wake.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 40, ni wachache ya baadhi ya wanamuziki wa injili waliosalia tangu kujiondoa kwa Willy Paul na Bahati ambao walizama kwenye nyimbo za sekula walizohisi zitawapa umaarufu zaidi.

Mimi sitaacha kuimba nyimbo za injili. Nina njia nyingi ya kujitafutia pesa. Niliitwa kuwa msanii kabla ya kuanza kuimba. Sitaki kamwe kuimba nyimbo za Sekula kama baadhi ya wenzangu walioimba injili wakati mmoja walibadilika,”  Alieleza Daddy Owen.

Baba huyo wa watoto wawili amesema kuwa kutulia kwake katika muziki si kwamba ameufisha muziki wake ila ni kutokana na majukumu na shughuli nyingi za kila siku zinazomkabili, huku akisema kuwa andaa kolabo na wasanii wengi wa injili na hivi karibuni atatesa anga.

Nimekuwa na shughuli nyingi, si kwamba nimepotea katika muziki. Kutetea haki za watu, kuzitetea haki za watoto walemavu na shughuli nyingine nyingi ambazo zimenikabili ndio sababu hamjanisikia kwa muda, ila siku zijazo nitatesa anga kama kawaida,” aliendelea kusimulia.

Kando na usanii, mwimbaji huyo amekuwa katika mstari wa mbele kuzitetea haki za binadamu, huku akizipa kipaumbele haki za watoto wanaoishi na ulemavu nchini akieleze kuwa pia nao ni binadamu kama wengine, na wana haki ya kupata malezi bora.

Owen, pia alikosoa vikali tendo la maafisa wa usalama kutumia nguvu kupita kiasi katika maandamano ya Julai 12, yaliyowaacha watu 9 wakiripotiwa kuiaga dunia, huku akidai kuwa huo ni ukiukaji wa haki za kibinadamu.

Kumpiga mtu risasi hadi kufa hakufai kabisa. Hizo ni dhuluma, huo ni ukiukaji wa haki za kibidamu. Badala yake maafisa wa usalama wangewakamata wanaoshukiwa kuwa waandamanaji na wawapeleke katika kituo cha polisi, waweze kufikishwa mahakamani ili mahakama itoe uamuzi,” Alisema.

Mwimbaji huyo alieleza kuwa kuna uhuru wa kujieleza kwa kila Mkenya, huku akilikashifu vikali tendo la maafisa wa usalama kumtesa na kumpiga vikali, jamaa aliyejifunga kwa nyuma katikakati mwa jiji la Nairobi huku akieleza hisia zake kuhusu uchumi wa taifa.

View Comments