In Summary

• Alifutilia mbali uwepo wa uhusiano wa kimapenzi na msanii huyo na kusema kuwa muziki tu ambao wanafanya.

• “Kuhusiana na Diana tunaenda kufanya tu wimbo na sitamtafuna,” alisema.

Diamond amsifia Spice Diana
Image: Instagram

Diamond Platnumz yuko nchini Uganda ambapo anatarajiwa kutumbuiza katika uwanja wa ndege wa Kololo usiku wa leo katika tamasha la vichekesho litakaloongozwa na mcheshi Alex Muhangi.

Msanii huyo alitua Uganda kwa kishindo akiwa na msanii mkongwe kutoka Kenya, Nameless na wengine wengi ambao watateka jukwaa la uchangishaji wa fedha kupitia tamasha la vichekesho.

Alhamisi alifanya mkutano na wanahabari katika hoteli moja alikotia nanga na aliweza kuwazungumzia wasanii mbali mbal iwa Uganda akiwemo Jose Chameleone na Spice Diana.

Diamond alisema kuwa anatamani sana kufanya kolabo na Chameleone lakini pia akafichua kwamba atatoa wimbo wake na Spice Diana kabla ya kurejea nchini Tanzania na hata ikiwezekana wafanye video na yeye kabla ya kuondoka.

Waandishi wa habari vile vile walimchokonoa kutaka kubaini ukaribu wa Spice Diana na lebo yake ya Wasafi ikizingatiwa kwamba amewahi fanya ngoma na Zuchu na pia Mbosso ambao wote ni wasanii walioko chini ya lebo ya WCB Wasafi.

Alifutilia mbali uwepo wa uhusiano wa kimapenzi na msanii huyo na kusema kuwa muziki tu ambao wanafanya.

“Kuhusiana na Diana tunaenda kufanya tu wimbo na sitamtafuna,” alisema.

Diamond alichafua hali ya hewa kabisa na kusema kwamba ikiwa litatokea jambo kati yao basi hakuna atakayelaumiwa kwani wao ni watu wazima.

“Lakini ukweli ni kwamba Diana ni mrembo na ikitokea kitu kimetokea si makosa yangu wala si makosa yake kwa sababu sisi wote ni watu wazima. Ni msichana mrembo ambaye si vibaya kupata mtoto naye,” Diamond alisema.

Kali hiyo inakuja siku moja baada ya kuonekana na mrembo mwingine wakiwa wamebarizi kwenye kochi na wengi walisema anafanya makusudi kumuumiza Zuchu ambaye aliwahi kukiri kuwa ni mpenzi wake.

 

View Comments