In Summary

• "Achana na kunilinda, huwezi nipigania. Nafikiri tunafaa kuacha kufanya hiki kipindi, nimeingiwa na stress,” Kamene alisema kwa butwaa na sauti iliyokosa matumaini.

• Wawili hao walifunga harusi mwezi Aprili mwaka huu baada ya kuchumbiana kwa karibia miaka mitatu.

Kamene Goro atema moto Bonez akisema hawezi kumpigania
Image: SCREENGRAB

Mtangazaji Kamene Goro alipandwa na mori kama Mmasai baada ya mumewe DJ Bonez kukiri kwamba hawezi kumpigania wala kumlinda anaposhambuliwa.

Katika Kipindi chao kifupi kwenye chaneli ya YouTube, Kamene Goro alimuuliza mumewe kama anaweza kujitokeza na kuchukua mkuki kwa ajili yake, jambo ambalo Bonez alikataa katakata akisema kwamba watu ambao hupigana ni kina Mike Tyson, gwiji wa mchezo wa ndondi.

Kamene alikasirika na hata kwa wakati mmoja kusema kwamba ni heri waache kuendelea ka kipindi hicho, akisema kwamba Bonez amebadilika na kusema hawezi kumpigania baada ya kuoana.

“Kwa hiyo mtu akinifinya makalio hutanipigania? Kwa hiyo huwezi nipigania? Huwezi nipigania? Ati ‘mimi siwezi pigania mwanamke’. Ni leo unaniambia kwamba huwezi kunipigania baada ya kuoana? Achana na kunilinda, huwezi nipigania. Nafikiri tunafaa kuacha kufanya hiki kipindi, nimeingiwa na stress,” Kamene alisema kwa butwaa na sauti iliyokosa matumaini.

Wawili hao walifunga harusi mwezi Aprili mwaka huu baada ya kuchumbiana kwa karibia miaka mitatu.

Wanandoa hao pamoja na mchekeshaji Oga Obinna wamekuwa wakifanya vipindi vya podikasti kwenye chaneli ya Kamene& Obinna haswa kila usiku wa Ijumaa kila wiki ambapo wanazunumzia mauala mbali mbali ya kimahusiano na familia.

View Comments