In Summary

• Katika ujumbe mfupi alioambatanisha na picha hiyo, alisema kwamba ni mwaka mwingine wa kujitambua na kujikuza.

BIRTHDAY Director Trevor ajinunulia zawadi ghali kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Image: INSTAGRAM

Mpenzi wa mwanablogu wa YouTube Mungai Eve, Director Trevor amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kujipaisha na kujifariji kwa njia nyingine tofauti.

Trevor kupitia Instastory yake, alipakia picha ya viatu vya rangi nyeupe na kupakia maelezo ya muamala wa M-Pesa ambai unaonyesha kiasi cha pesa alichotoboka ili kupata viatu hivyo.

Katika muamala huo, Trevor alionyesha kwamba alitumia shilingi elfu 50 ppesa za Kenya kununua viatu hivyo kama zawadi ya kujifariji na kujisherehekea kwa kuvuka mwaka mwingine katika maisha yake.

Katika ujumbe mfupi alioambatanisha na picha hiyo, alisema kwamba ni mwaka mwingine wa kujitambua na kujikuza ambao aliona ni vyema kujinunulia zawadi hiyo ghali katika kile alisema kuwa nata thamani yake mwenyewe inaridhia na kuikidhi zawadi hiyo.

“Hongera kwa mwaka mwingine wa kujipenda mwenyewe na kujikuza. Nasherehekea siku yangu ya kuzaliwa kwa kujinunulia zawadi ghali kwa sababu thamani yangu mwenyewe inakubali,” Trevor aliandika.

trevor ,mungai eve

Kwenye picha hiyo, aliweka wimbo wa Afrobeats wenye maudhui kwamba katika maisha haya mtu hufai kujipa shinikizo katika vitu vingine, mengine ni ya kuacha tu yapite na ujiburudishe katika yale ambayo unayaweza kuyakidhi.

Kwa haraka tu, mpaka Makala haya yalipokuwa yanachapishwa, mpenzi wake Mungai Eve hakuwa amemuandikia ujumbe wowote kumsherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kando na kuwa wapenzi, Trevor ndiye muongozaji mkuu wa video ambazo wanafanya za kuwahoji watu na kukuza maudhui.

View Comments